Wednesday, February 22, 2012

JESHI LA POLISI LATUMIA SILAHA ZA MOTO KUTAWANYA MAANDAMANO YA WANANCHI SONGEA

Polisi wakiwa katika gari lao wakati wakutuliza vurugu zinazoendelea wakati huu mjini Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo kuandamana kupinga mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na watu wasiojulikana.

Polisi wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji.
MADEREVA PIKIPIKI WAKIWA WAMEFUNGA BARABARA YA SONGEA KWEWNDA TUNDURU KARIBU NA MLANGO WA KUINGILIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA Ruvuma,wakilitaka jeshi la polisi mkoa huo kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya watu yanayoendelea mjini songea ambapo hadi sasa zaidi ya watu 8 wameuawa na watu wasiojulikana wengi wao wakiwa ni madereva wa pikpiki.

NA MUHIDIN AMRI,SONGEAJESHI la polisi mkoani Ruvuma limelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wananchi waliokuwa wakiandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma na kituo kikuu cha polisi Songea mjini hali iliyopelekea shughuli mbalimbali kusimama.Hali hiyo ilianza kujitokeza majira ya asubuhi ambapo wananchi wa mtaa wa Lizaboni wengi wakiwa ni madereva wa pikpiki walianza kujikusanya na kuanza maandamano kuelekea kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu na uwanja wa majimaji mjini hapa.Wananchi hao walikuwa wakiimba nyimbo za kulaumu jeshi la polisi wakidai kuwa limeshindwa kudhibiti mauaji yanayoendelea kujitokeza mjini hapa kila mara ambapo hadi sasa zaidi ya watu kumi wameshauawa na watu wasiojulikana.“Tumeamua kuandamana kwani kimsingi mauaji yamezidi kutokea mjini hapa jana ameuwawa mtu,juzi na usiku wa kuamkia leo ameuwawa mwendesha pikipiki na abiria wake”walisikika wakisema.Baada ya wananchi hao kukaribia kituo cha polisi walianza kurusha mawe na ndipo polisi walijihami kwa kutumia mabomu ya machozi ambapo wananchi hao na waendesha pikipiki walianza kukimbia ovyo na kupeleka maduka kufungwa kwa hofu ya kuibiwa.Licha ya biashara mbalimbali kusimama pia ofisi za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa na ya mkuu wa wilaya Songea zilifungwa kwa kuhofia waandamanaji kuingia kwenye ofisi hizo na kufanya uharibifu.Kabla ya maandamano ya leo februari 20 mwaka huu wananchi kutoka kata ya Lizabon waliandamana hadi kwa mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Ole Sabaya kulalamikia kukithiri kwa mauaji katani humo ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana.Akijibu malalamiko hayo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa serikali itahakikisha ulinzi unaimarishwa na kwamba aliwataka kuimarisha ulinzi shirikishi ili kukabiliana na matukio hayo maovu.Februari 19 mwaka huu mkazi wa Lizaboni Bakary Ally(20) aliuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana ambapo februari 20 mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku mtu mmoja mkazi wa mtaa wa Kipera shekhe Jamari(65) alikutwa ameuwawa kwa kukatwa mapanga kichwani na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akielekea nyumbani kwake.Marehemu Jamari alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wa msikiti uliopo katika eneo hilo la Kipera.Mauaji hayo yameendelea kujitokeza ambapo mwendesha pikipiki ambaye jina lake halikufahamika mara moja ameuwawa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Mji Mwema mjini hapa usiku wa februari 22 mwaka huu na kupelekea wananchi mjini hapa kuishi kwa hofu kubwa.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimepatwa na wasiwasi pia uchungu kwa Songea yetu ndogo kupatwa kwa majanga kama haya. Napenda kumwomba Mwenyezi Mungu awashushie amani. awape marehemu mwanga wa milele:- amana

sam mbogo said...

Bila shaka serikali itashughulikia tatizo hili,kwani kila lililo na mwanzo halikosi kuwa na mwisho.watanizangu wangoni kutakuwa nataizo mahali ,kama nikikundi, au nimtu basi arobaini zake zaja msihofu tuko pamoja katika shida na raha,poleni sana. kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Ahsante kwa kututia moyo watani wako. Ni kweli za mwizi arobaini..ila tu inashangazi Songea yetu iingiliwe hivi kweli?

SIMON KITURURU said...

Ila TANZANIA tunakokwenda wala sio salama - kwa mwendo huu!:-(

Mija Shija Sayi said...

mmmmhhh..

sam mbogo said...

Nimejaribu kufuatilia swala hili,hasa kutoka katika maelezo alio sema mkuu wa mkoa,kwamba mambo yote haya nisababu ya imani za/ya kishirikina.!? lakini ukienda mbali zaidi kuna swali la kujiuliza kama ndo hivyo kwanini serikali hasa huyu mkuu wa mkoa hakusema na wananchi haya anayo yasema leo? matokeo yake wananchi wameona kimya wakaamua kuingia barabarani. uwajibikaji wa viongozi wetu ni duni sana,kama usemavyo mtakatifu tunako kwenda mwisho wake itaigharimu nchi. kaka s