Saturday, February 11, 2012

JUMAMOSI NJEMA JAMANI LEO TUSIKILIZE NGOMA YA ASILI YA WAHAYA WA KAGERA NA DADA SAIDA KAROLI


Saida Karoli ni mmoja wa wasanii niwapendao sana hata kama kuna nyimbo nyingine anaimba kilugha na sielewi lakini naridhika kabisa. Nadhani ndio maana napenda, halafu ni ule uasili, utamaduni wetu au niseme kwa ujumla napenda sana vitu vya ASILI. Na naamini kuna wengi wa aina yangu. Je wewe kuna msanii umpendaye?

6 comments:

ray njau said...

Kajitahidi sana kulingana na uwezo wake.Mimi nawapenda sana wagosi wa kaya kwa kuweza kuimba katika lugha ya Kiswahili chenye lafudhi ya wakazi wa mkoa wa Tanga.
-----------------------------------
Angalizo:
Wanamuziki wa Tanzania wanashindwa kupenyeza kwenye anga la kimatifa kutokana na ukosefu wa ubunifu.
----------
Ushauri:
Wekeni mashairi yenu katika lugha za makabila yenu mkipenda.Na mashairi hayo yawekeni tena katika lugha ya Kiswahili,Kiingereza ,Kifaransa na lugha nyinginezo nyingi mkipenda.
----------------------------------
Hitimisho:Ukiimba kikabila tu katika hizi zama za teknohama unabakia nyuma ya mshale wa saa.Twendeni kitaifa na kimataifa zaidi chini mwamvuli wetu wa asili.
===================================
"HAKIKA JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI"
-----------------------------------
SHUKRANI:Kwa mwenye blogu pokea shukrani na salamu zangu na kwa wadu wote kwenu nasema wikiendi maridhawa kifamilia zaidi.

Rachel Siwa said...

Mimi napenda sana miziki mingi tuu yenye uasili hata ngoma pia napenda pia,kifupi napenda na kucheza pia,hapa nilipo nipo hoi na huu mziki wa leo, kama ningepata katogwa kidogo ili roho ipoe, Ohhhhh iiii.J'mosi njema na wanangu na baba yao pia, nawooote!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Tuelimisheni nasi waBondeni kidogo.

Ni "Wayawa" au "Wayahawa", au hao ni makabila mawili tofauti, au vidole vimeteleza kidogo kwa Mdogo wangu?

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana nawe kaka Ray..halafu nimependa kweli msemo huu "HAKIKA JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI"

RAchel unaweza kupitana na mimi kuimba au kucheza miziki ya asili?
Nimefurahi kusikia kuwa unacheza na ungepata katongwa haya pokea hiyooooooo:-)

Kaka mkubwa Phiri! nimesawazisha Ahsante!

Rachel Siwa said...

Dada yangu Kuimba duh naona Mungu alisahau kuniingiza kwenye chumba hicho, sauti ya kuimba 0 juu chini chini juu tehtehtehte,yaani naimba kujifurahisha tuu, lakini si muimbaji dada.Kucheza dada YaSinta mpaka waseme jamanieee basiii mziki/Ngoma unazimwaaa hahahaahhahah!!nafikiri hapa dadake nakutoa/kukushinda,hahahha,Ahsante kwa TONGWA DADA YANGU,Swali la Kizushi jee unajua KUPIKA/KUTENGENEZA TONGWA?

Yasinta Ngonyani said...

Rachel una vituko wewe nimecheka kweli hapa haya basi itabidi tuanzishe kwaya yetu unasemaje?
KUPIGA TONGWA MMHH NISEONGOPE SIWEZI AIBU KWELI ETI EEEEHH!!