Wednesday, February 29, 2012

MADONGA/NATURAL TROPICAL FOREST FRUITS......



MADONGA/MATUNDA YA ASILI
Nimeamka nikiwa na hamu kweli ya matunda haya ya asili, nimekumbuka nilipokuwa mdogo ukienda mstuni kuokota kuni basi huko nyumbani wasahau maana chakula tayari kilikuwepo. Matunda haya yanakuwa kwanza kijana, na baadaye yanakuwa njano unapasua na ndani yake kuna mbegu. Mbegu hizo zina nyama nyingi tu basi unazimungúnyamungúnya kama vile pipi na mbegu unatema...weeeeeeeeeeeee ni matamu na sijayala miaka mingiiiiiiiiiiii nimetamani kwelikweli...kama vile LIKUNGU....Kuna mwingine amewahi kula matunda haya????

10 comments:

Rachel Siwa said...

Mimi sijawahi kula da'Yasinta,lakini natamani nionje.

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! fuatana nami siku yake tukaokote kuni halafu uone kama utarudi mapema:-)

batamwa said...

yaani katika watu wanaoturudisha enzi za ujana ni wewe dada yasinta ubarikiwe sana

Simon Kitururu said...

Matunda matamu haya ila DADA yangu akila haya anavimba!


Katika uchokozi:
Hivi ni tunda la asili walilokula Adamu na Hawa?

Rachel Siwa said...

Nitafanya hivyo dada yangu, ili nami nionje,@kaka wa mimi KITURURU mwanaaa Tunda walilokula Adam na Hawa? Tehtehthetheteeeeeeeeeeeeeeeeeee

Yasinta Ngonyani said...

Batamwa Kwanza karibu sana. Pili nafurahi kama umeweza kurudi nyuma enzi za uajana..nahisi nami nimekumbuka hivyo pia.

Simon! kumbe umeyaanja eeh! pole na dada kwa kukosa uhondo...Simon nadhani ilikuwa hivyo tunda walilokula Adamu na Eva ni TUNDA LA ASILI
Rachel! Yaani utayapenda na hutaonja tu utakula mpaka kuvimbiwa nakuambia:-)

sam mbogo said...

Matunda utamu wake uya fuate porini. mfano sisi tuliokulia kijijini kipengere cha kutafuta kuni mnakuwa wengi tu mchanganyiko wavulana na wasichana,porini panakuwa hapatoshi!!,we acha tu Yasinta umekumbusha mbali sana. kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Kuishi kijijini ni urithi mzuri sana na ni kufaidi vitu/vyakula vingi sana vya asili..na halafu unakuwa na afaya njema na ngangali nayakumbuka sana maisha yale...

Nampangala said...

Ni kweli kabisa utamu wake uyafuate polini. mlongo umenikumbusha mbali sana sana sikuweza kuacha kucheka mala tu nilivyoiona hii picha ya madonga. we acha tu kwakweli tumetoka mbali. Asante mlongo ubarikiwe sana

Anonymous said...

Asee haya matunda yanapatikana sana huko songea maeneo ya lilondo ni mazur sana nimefika Tabora nimeyakuta nimenunua ndo nakula sasa hivi hapa