Sunday, February 5, 2012

JUMAPILI NJEMA...KARIBUNI CHAI KWA MIHOGO YA KUCHEMSHA!!!!

Mihogo ya kuchemsha.......
Na chai ya rangi

Karibuni tujumuika, mimi napenda zaidi mihogo ya kuchemsha. kuna wengine wanapenda ya kuweka nazi, karanga au nyanya na vitunguu. Je wewe unapenda mihogo yako itayarishweje? Haya ngoja niwatakieni wote jumapili njema sana. Mimi nakunywa chai yangu hapa maana baridi si mchezo!!!!

18 comments:

Mija Shija Sayi said...

Yangu ikaangwe...na pilipili mmh!! Jumapili njema wote.

sam mbogo said...

Nyinyi akina dada hamlali tu,saa hizi mbona siku yajimapili bado,we Mija tafadhali umepona baridi kaka s

Rachel Siwa said...

Tehtehteh kaka Sam my barafu!bora uwaambie hao baridi hii wao wanablogu tuu badala ya kuwa na waume zao,sijui wanatufunza nini sisi wadogo zao!! Mimi nimechungulia kwa sim tuu,nipo mzigoni mwayego,hiyo mihogo kwangu mimi jamani vyovyote tuu hata Makopa mimi nakula,mnayajua Makopa? Mbarikiwe woote na J'2 njema.

shekhe said...

Mi napenda wangu uliwe mbichi pasi nazi wala mafuta

Mija Shija Sayi said...

@Rachel..Mke wa Kaka S anajua kiswahili ni balaa, sasa wewe endelea kumwita kaka s my barafu..mimi simo!

Kaka S, tupone wapi? Hiyo snoo yake si mchezo halafu sikuwepo nyumbani. Vipi huko mmepona? Yainta nyie theruji vipi?

Rachel Siwa said...

Jamani da'Mija kwani Barafu si barafu au?tehtehteh

sam mbogo said...

Hivi huo muhogo niana gani ya mhogo.kuna mhogo wajang'ombe,nk mimi hupenda mihogo ya kukaanga chipsi dume,nakumbuka enzi hizo tukao tambaza, mihogo tlikuwa tuna nunu pale muhimbili shule ya msingi,tuna shushia na potelo(juisi) kutoka kidukashop!. unajuwa bisikuti yangu(Rachal) hapa nilipo barafu yako nimeganda nasubiri kijua kitoke nipate kuyeyeuka. ulaya nikutam lakini haya mabo ya barido! we acha tu afadhali wliokuwa wana blog usiku akina.......!? utanimwinginene lakini,haya dada zangu wala msikonde tuko pamoja. mija nakutafuta sanaa. kaka s

Interestedtips said...

hiyo mihogo nimeitamani,inaonekana mizuri hasa

Mija Shija Sayi said...

@Kaka S, njoo facebook ukutane na wasanii wenzio nakuhakikishia hutapachukia..

sam mbogo said...

Dada yangu Mija,facebook!? hatasikumoja. nimepoteza contact zako ninazo za zamani,mail nimekutumia lakini naona kimya. haya jumapili njema. kina kili na Oscar wanataka kukutembelea.kaka s

Baraka Chibiriti said...

Mimi ni mgojwa wa Chai tu, yaani niheri uninyime vyote kuliko chai.

Asante nawe pia Jumapili njema!

Mwanasosholojia said...

hukrani Da'Yasinta..pole kwa baridi, tunapambana nayo si mchezo!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni sana wote kwa maneno yenu mazuri. Na halafu labda niseme hivi hapa ni kwamba huwa nategeshea mada au kitu na kuchagua muda na halafu kinajipublisha muda ukifika. Mija baridi ipo yaani ukitoka nje pua yote inajikunja na mafua yanatoka bila hata kuwa na mafua...kaka Baraka basi tuko wengi mie ninyime chochote ila si chai---kaka Mathew ulipotea kweli ni furaha umerudi:-) ruksa kuendelea kujadili mihogo na chai!!

ray njau said...

Chai ndiyo urithi wetu na mihogo ina wenyewe.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray Una maana gani mihogo ina wenyewe? wewe huli mihogo?

Anonymous said...

Aka lakini mihogo inaonyesha haikuwiva sawa da yasinta au umefanyia haraka huko jikoni

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wala usiogope kuja kula umeiva tena ina unga hiyo.

Mwanasosholojia said...

Dada yangu mapambano tu, mnisamehe kwa kimya kingi..:-)