Thursday, February 9, 2012

HIVI KWANINI WANAPOJENGA/TENGENEZA HIZI BARABARA HAWATENGENEZI NA BARARA ZA BAISKELI.....

.....Maana hii ni hatari kwa wananchi kuendesha baiskeli hivi fikiria sasa hapa magari mawili yanakutana je huyu kijana maisha yake yataweza kuokolewa kweli? Ni wazo tu la leo.....

6 comments:

Mcharia said...

HIVI KUNA LESENI ZA KUENDESHA BAISKELI? KAMA HAKUNA NI KWA NINI.

Inabidi kujiuliza ili tuwe na uhakika wa kuwepo barabara za baiskeli.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mcharia! uwepo wa barabara za baiskeli ni muhimu sana kwani ungepunguza vifo vingi tu vya waendesha baiskeli na watembeaji pia. Kama umewahi kufika Songea/Bombambili pale kwenye ule mlima wamekufa watu wengi sana kwa kuendesha baiskeli katikati ya barabara....

ray njau said...

Kule Unguja swali hili halina majibu kwa kuwa barabara moja ni kwa ajili ya wote.
Lakini sina hakika sana iwapo tunafahamu gharama za ujenzi wa kilomita moja ya barabara ya lami.Hapa uwezo wa nchi yetu kiuchumi unafanya tukubaliane na usemi huu:"KATA KOTI LAKO KULINGANA NA KITAMBAA CHAKO".Hapa tushukuru kwa tulichopata na tuwe waanaglifu katika matumizi ya barabara zetu.

Baraka Chibiriti said...

Sio tu barabara za waendesha baiskeli, pia parking katika barabara zetu, hamna kabisa. Kwamfano Barabara kuu ya Dar - Dodoma, ambayo mimi hupita kila mara...ina karibu KM 500, pia ile ya Morogoro - Mbeya, lakini hauoni Parking kabisa, je ukichoka kuendesha gari, unajisikia usingizi unapaki wapi?au kuharibikiwa na gari... Yaani kama una busara lazima utafute sehemu uliingize gari porini, ambapo wengi hawafanyi hivi,wanayaacha magari yao barabarani ovyo tu ndipo unaona ajali nyingi zinatokea karibu kila siku...kutokana watu wanapaki ovyo ovyo magari yao...hakuna Parking, na wengine wanayavamia kwa kuyagonga. Tanzania yetu bado sana elimu ya barabarani, ndio maana unaona hata wanapojenga barabara hawaweki vitu muhimu kama hivyo, sijui viongozi wetu hawaoni na kujifunza wanapokuja nchi za wenzetu au makusudi tu? Kila siku lazima watu wafe kizembe zembe barabarani bila sababu yoyote.

Mija Shija Sayi said...

Sisi tumefuata mfumo wa UK. Yasinta siku ukijanitembelea utasema, barabara ndogo ndogo na wote humo humo. Ukikaa nchi zingine halafu ukaja Uingereza utalia...

Yasinta Ngonyani said...

Wote nafurahi kila mara mtoapo michango yetu. Mija nitakuja we ngoja tu:-)