Friday, February 10, 2012

Je? ulijuwa maana ya jina la mji wa MOSHI/Sala za Wachagga kulingana na eneo wanalotoka (utani)

Sala Kuu:
MOSHI: Mungu Onesha Sehemu Hela Iko

Viitikio:
1. Hata Ikipungua Mungu Ongeza! (HIMO)
2. Mungu Angalia RAia NGawira Utuhakikishie! (MARANGU)
3. Mungu Ahidi Mapesa Bila Ajira! (MAMBA)
4. Mungu Wekeza Ishara Kwenye Akaunti! (MWIKA)
5. Kristu Imarisha Leo Elimu na Mapesa Akauntini! (KILEMA)
6. Kristu Imarisha Riziki Ujaze Akaunti! (KIRUA)
7. Usitunyime Riziki Uchumi! (URU)
8. Kila Ikipungua Baba Ondoa Siasa Hela Ongeza! (KIBOSHO)
9. Mungu Atupe Chanzo Halisi Ambacho Mapesa ni Endelevu! (MACHAME)
10. Kwetu Ikikosekana SHIlingi MUngu Nakuapia Dunia Utaichukia! (KISHIMUNDU)
Kaaaziii kwelikweli!!Nimecheka kweli mpaka nimepata maumivu kwenye mbavu hii chanzo chake ni Subi

5 comments:

ray njau said...

Hapa leo kisu kimegusa mfupa.Naawachia wenye meno watafune.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nimecheka ukizingatia nimewahi kuishi moshi! sehemu hizo zote nimefika!

ray njau said...

Kwa waliosoma jiografia ya Uswiswi hawawezi kuwashangaa sana wachagga kwa kuwa mazingira huzaa tabia fulani ambao wengine huenda wakaona ni komedi.Kutokana na jiografia ya Uswiswi wao hutegemea zaidi usafiri wa anga na hivyo wakawa wabunifu na wauzaji wazuri wa kamera na saa.
Wingi wa wachagga na ufinyu wa ardhi yenye rutuba ifaayo kwa maisha endelevu umeyafanya maisha ya uchaggani yategemezwe na pesa.Kwa ujumla sasa wachagga wanaweza kuishi katika mazingira yoyote na kujichanganya na makabila mengine katika familia na tamaduni zao.
===================================
HITIMISHO:
Kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani sasa hakuna tena cha mchagga wala asiye na kabila katika mikikimikiki ya maisha na mafanikio.

ray njau said...

Kunradhi:
Jiografia ya[switzerland]Uswizi.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni Ray na Kamala kwa mchango wenu..Mie nilibaki hao kucheka si kucheka kaaaaazi kwelikweli hapa duniani katika haya makabila