Sunday, February 19, 2012

LEO NI JUMAPILI MAALUMU KIDOGO KWA KAKA YANGU SAVIO /BABA AHSANTE ANATIMIZA MIAKA HONGERA KAKANGU!!

Huyu ni kakangu, Savio Ngonyani/baba Ahsante ambaye alipokea ziwa/titi baada ya mimi na leo ni siku yake ya kuzaliwa ametimiza miaka kadhaa. Savio napenda kukutakia kila la kheri katika siku yako hii ya kuzaliwa. Wote hapa katika kaya hii wanakutakia kila la kheri. Kwa vile najua wewe ni mwanakwaya na halafu Kwaya master basi nakuwekea wimbo huu halafu kikundi cha kwaya ni kama jina lako...

HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKANGU. NA KUMBUKA YA KWAMBA WOTE TUNAKUPENDA.

6 comments:

SIMON KITURURU said...

Hongera Papaa Savio Ngonyani!Kula bata aisee ikiwezekana kwa kuwa MAISHa ni mafupi aisee MKUU!!

Tukiachana na hilo,...
JUMAPILI NJEMA Wadau wa KIJIWE HIKI!

Mija Shija Sayi said...

Nakutakia heri ya siku ya kuzaliwa Kaka Savio, Mungu awe azidi kukujaalia afya na maisha mazuri..

Happy birthday.

Anonymous said...

Heri ya kuzaliwa kaka yetu.tunatumaini umeifurahia siku yako hii.mwenyezi mungu akuongezee miaka mingi zaidi ya kusherekea siku yako ya kuzaliwa.Ubarikiwe sana.
mlongowo.

PASSION4FASHION.TZ said...

Hongera kwa kutimiza miaka kazaa kaka Savio,mungu akuongezee miaka mingi zaidi.

Rachel siwa Isaac said...

Hongera sana kaka Savio,Mungu akuongezee miaka mingi yenye baraka na Amani.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote mlikuwa nami kwa kusherehekea siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kakakangu.
AHSANTENI