Thursday, February 2, 2012

NATAMANI KUWA MDOGO NA MREMBO KAMA HAWA WATOTO

Natamani kuwa mdogo tena, angalia watoto hawa walivyopendeza NIMEIPENDA SANA PICHA HII NA NIMEONA IWE PICHA YA WIKI HII.

8 comments:

ray njau said...

Siku hazingandi lakini zinayeyuka.

Yasinta Ngonyani said...

Haswaaaa kaka Ray...kuwa mdogo ni raha sana maana huwi na majukumu mengi kila kitu unafanyiwa...Halafu hii picha inanikumbusha mbali sana ila mie nimecheza sana na kaka zangu. Ila hao sijui wanakwenda wapi angalia upensdo ulivyoenea kati yao mpaka raha:-) Na haya magauni yao ama kweli hao ni warembo wa wiki katika blog hii.

sam mbogo said...

mimi nimependa hasa HIRIZI shingoni ya huyo mtoto wa upande wa kushoto. watu husema watoto ni malaika,japo wanahirizi!!? kaka s.

Baraka Chibiriti said...

Mbona wewe tayari Mrembo Dada Yasinta....unataka uwe mrembo mara ngapi? Labda useme unatamani kuwa mtoto, hapo sawa.

Lakini hilo haliwezekani, hata mimi natamani sana kuwa mtoto tena, maana utoto ni raha tupu, ukubwa shida tupu.....kazi kweli kweli!!!!

Anonymous said...

Kwa nini?

Tatizo ni muda...

Muda si muda hawa nao watakuwa vikongwe kama wewe !!!!

emu-three said...

Maisha ni kama maji ukiyamwaga hayazoleki, ni kweli kama ingeliwezekana maisha yakawa kama comupta, unaweza ukapreview, au .....oh, mungu mkubwa

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! kuna siku nilikuambie utumie miwani lakini sasa naona acha tu yaani umeona hadi hirizi. Ndio watoto ni Malaika ndo maana nami nataka niwe mtoto tena..LOL

Kaka Baraka! umenivunja mbavu Ahsante...kuwa mtoto raha kweli ila sasa ndo tunakuwa watoto/wazee

Usiye na jina ! kwa sababu kuwa mtoto ni raha..na kuwa mkongwe ni majukumu mengi:-(

emu3! kweli maisha ni kama maji...ni furaha kuona upo.

Nicky Mwangoka said...

Watoto wadogo wanikumbusha uwepo wa Mungu sana katika maisha yetu. Hongera kwa post ya picha hii ya watoto wapole na wanyeyekevu