Friday, February 24, 2012

UJUMBE WA LEO:- KILA BINADAMU ANA MAPUNGUFU YAKE!!!

Sisi binadamu tumeubwa na mapungufu, Hakuna aliyekamilika kila mmoja ni tofauti na mwingine. Kuanzia kimawazo, kimatendo pia kitabia. Na kwa kuwa kama tulivyo, hii ndio maana tuna hitaji pale jambo linapopinda, tuchukue jukumu na kujaribu kuliweka sawa na pia KUSAMEHEANA. Ila KUMSAMEHE mtu si jambo dogo maana kama kweli unamsamehe mtu basi umsamehe KIDHATI/TOKA ROHONI. Au hata kumpa yule mtu aliyekosea/uliyepishana naye mawazo nafasi ya pili/ajaribu tena. Sababu yeye ni banadamu kama wewe, yule, mimi na wao. NACHOTAKA KUSEMA:- KAMA UMEHITILAFINA NA MTU JARIBU KUONGEA NAYE ILI KUSHULUHISHA NA UTAOANA MAISHA YANAKWENDA SAFI. KWANI KUKAA NA KITU MOYONI HAISAIDII KITU. Binafsi kama kuna kitu nimemkosea mtu/nimemdanganya mtu basi NASEMA SAMAHANI SANA kwani hata mie ni binadamu na nina mapungufu.NA NINGEOMBA TUANZE UPYA/SECOND CHANCE. IJUMAA NJEMA!!

5 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

imani yako imekuponya, enenda zako umesamehewa dhambi zako!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Chacha! sikujua kama wewe ni Padiri! Ahsante.

sam mbogo said...

Nakubaliana na wewe,kila binaadamu ana mapungufu yake. swala lakujiuliza niwakati gani twaweza kugundua mapungufu yetu hayo.?zamani nilikuwa naweza kumlaumu mtu kwa kuchelewa kuja ,hasa kama tumeahidiana. sasa hivi wala sipotezi muda ju ya jambo hilo,kwani kutokufika kwa mtu huyo ,kuna mawili,moja yaweza kuwa nibahati mbaya kunakitu kimetokea ambacho hakukitegemea. na pili wenda ni uzembe tu. hivyo kwahilo lakwanza nitakuelewa na kukusamehe hatakama hujasema.la pili pia nitakusamehe kwa sababu umeniwezesha kukujuwa wewe nimtu wa ainagani. huo ni mtazamo wangu katika kuielewa jamii na watuwake. kaka s.

Anonymous said...

Da Yasinta, wengine wanasema "Word!" kwa uliyosema. Tena, kukaa na kitu moyoni bila kukitoa, ni kujisambazia mwilini chembechembe zilizojaa negative energy. Inakuumiza mwenyewe.

ray njau said...

Kusamehe ni kusahau na kamwe usiseme nimekusamehe lakini sitasahau.Nami nasema samahani kwa wote na nawasamehe wote.