Friday, February 3, 2012

NIMEWASIKIA WENGI WANASEMA UKITAKA KUJUA MENGI BASI NENDA KWENYE VILABU VYA POMBE.....

.....Lakini kumbuka pombe si maji kunywa kidogo isije ukashindwa hata kujua chochote kilichozungumzwa. Ukinywa kidogo utaepuka ajali na pia utatunza afya yako. Unajua kwamba mnywaji pombe sana anazeeka kwa haraka kuliko asiyekunywa?

5 comments:

ray njau said...

Hapa namkumbuka nguli mmoja wa muziki wa dansi nchini Tanzania aliimba:"POMBE SIYO CHAI".Katika media za Tanzania kuna matangazo yanayoendelea kusika hewani na kuishia na kibwagizo:"ULEVI NOMA".
-----------------------------------
Wanywaji-walevi hawana mapenzi na chakula na pombe imekuwa ndiyo lishe-maisha.Kwa hali hii uzee wa kuchakachua haukwepeki.

Mija Shija Sayi said...

Unajua watu karibu wote kama sio wote ukiondoa watoto, tunaishi kinafiki. Hapa nina maana kwamba watu wanavyotuona nje sio tulivyo ndani...hii ni kwa sababu ya kuepuka kukwazana, sasa pombe huondoa hii kitu ya kufichaficha mambo, humweka mtu huru zaidi na ndio maana katika ulevi kuna kukwazana kwa hali ya juu kitu kinachopelekea ugomvi usoisha.

Sasa basi kwa vile pombe huondoa chembechembe zote za kufichaficha mambo, nakubaliana na wewe kabisa Yasinta huko vilabuni kuna mengi ya kujua na kujifunza maana hakuna siri.

Swali je pombe idumu?

Anonymous said...

mija pombe idumu hivi chukulia kusingekuwa na pombe watu tungepata nini cha kutu badirisha mawazo yaani kutuchangamsha!!maana ukienda msikitini au kanisani habari za huko ni ukifa unaenda motoni yaani vitisho tu lakini pombe aa unakunywa unaburudika basi fuja mali kufa kwaja

Simon Kitururu said...

Hivi kwanini watu huofia kuishi maisha mafupi? Mara kiduchu huwa nashangaa nnikisikia watakao kuishi maisha marefu hasa kwa kuwa waliokula chumvi sana sijawahi kuwaonea wivu hasa baada ya kuwasikiliza na kushuhudia hata pale wageukapo kuwa shughuli kiafya au tu hata kivingine!
Nni moja ya mtazamo tu huu!

Sifagilii POMBE ila nsikufiche- naiamini kuliko watu wengi sana kwa kuwa ki asilimia mima naielewa itaniamsha nyege gani!

Anonymous said...

super myakaya