Thursday, January 26, 2012

JE? KUNA NAFASI YA KUKIMBA HAPA?

Kaaaazi kwelikweli hilo panga hilo, kweli siku ya fumanizi ni fumanizi au niseme za mwizi orobaini!! Sijua hapo mwenye kosa ni nani? Maana inaonekana kama huyo mume mwenye panga hapo ndIo nyumbani kwake na ameibiwa. Mmmmmhhh!

13 comments:

ray njau said...

Mshuko wa maadili ndani ya jamii ndiyo matokeo kulegea kwa vifungo vya ndoa na zinaa kuingia kwenye anga la promosheni.Ni kweli kuwa ndoa ni mkataba wa hiari kati ya wawili ambao kwa ridhaa njema wameamua kuingia katika kifungo cha ndoa lakini iwapo mmoja kwa ridhaa yake anaamua kuondoka kupitia uvunjaji wa maadili ya kiapo cha ndoa ni vema busara itawale sheria.Usilaumu ulipoangukia bali ulipojikwaa.

Swahili na Waswahili said...

Wote wanamakosa da'Yasinta huyo bibi na bwana pia, waliofumaniwa,yaani sijui kwanini watu wanapenda kusalitiana, tena utakuta mwingine unacheka naye na kumuona mtu wa karibu yako/Mpendwa mwenzio kumbe anakula kisogo,Lakini dunia haina siri ipo siku ndiyo kama hivyoo.@kaka Rau ahsante kwa maneno mazuri,Mungu azidi kukubariki.

ISSACK CHE JIAH said...

JUZI ILIKUWA MWANA KAMBAKA MAMA ,LEO NI FUMANIZI HAPO MOJAKWAMOJA DUNIA IMEKWISHA ILA HAPO HAIFAHAMIKI NI WAPI NA NINI KILICHOJIRI,HAPO KWA MAWAZO YANGU HUYO MWENYE PANGA NI JAMBAZI KAMSUBIRI JAMAA KATOKA SAFARI BAADA YA KUFUNGULIWA MLANGO NA MKEWE WAKATI WANASALIMIANA JAMBAZI KAMWINGILIA KWANI WALISAHAU KUFUNGA MLANGO WAO HUYU KAJUA KUWA JAMAA ANA PESA KWAVILE AMETOKA SAFARI HUYO MWENYEPANGA NI JAMBAZI TUU TUSIMJAJI KAMA JAMAA NI MGONI LA HASHA JAMANI ONENI HII PICHA MIMI NDO HISIA ZANGU KWANI KAMA WALIKUWA KWENYE NYUMBA YA WAGENI BASI WOTE WANGEKUWA WAPOWAPO TUU,CHE JIAH

ray njau said...

@Swahili binti Waswahili;
Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.
Shukrani na asante ni mapacha wa maisha na mafanikio.

sam mbogo said...

.muhimu hapa ni kudhibiti tabia ambayo mke/mume aweza kuwanayo na ambayo ukifuatilia waweza ukagundua kuna sababu kwanini mume/mke katoka nje na kafumaniwa.kaka s.

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Anonymous said...

Makosa ni ya wote kwakweli mke astahili kuwa mke na huyo mwanaume kama ana mke huko kwake hastahii kuwa mume maana ndoa yapande zote mbili imekwisha na siyo kwa hao tu bali ni kwa wanandoa wowote wale kama unajua unako hako kamchezo na ni mwana ndoa hauna ndoa tena nikimaanisha ndoa yako ni batili, hata biblia inasema wazi ya kwamba si baba ,mama au ndugu watakao weza kuivunja ndoa isipokuwa kwa tendo la zinaa na lo ndilo hilo,jamani wapendwa wenzangu tuwe makini.

sam mbogo said...

sawala hapa ni adhabu,au hilo panga ambalo kwa hakika huyo bwana anaelekea kumdhuru mtu,je nihaki huyo jamaa kumkata mapanga huyo mwanaume?.kosa lisha tendeka,lakini nikwanini maranyingu mwisho wa mamboyote haya utasikia ,fulani kampiga risasi mtu aliye mfumania na mkewe,au wanawake wagomabana na kuachana uchi baada ya mwana mke kumfumania mumewe.je inasaidia mke/bwana kutorudia tena kosa hilo baada ya adhabu aliyo pewa? kakas,

Mija Shija Sayi said...

Kichwani mwangu naona kama ni baba amemkamata mwanae na boyfriend.. na ndio maana huyo binti haonyeshi kushituka kihivyo..

Mija Shija Sayi said...

Kichwani mwangu naona kama ni baba amemkamata mwanae na boyfriend.. na ndio maana huyo binti haonyeshi kushituka kihivyo..

ray njau said...

Upanga wa binadamu ni wenye madhara ya muda yanayoweza kutibika au yasiyotibika lakini madhara ya upanga wa Mungu ya milele kwa waasherati,wazinzi na wadau wote wa ngono zembe.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

MH haya ni maigizo. mwanamke yuko uchi, kashikilia kishuka tu harafu mwanaime kava kabisa tena jinzi, kaivaaje haraka haraka?? hili ni igizo kuliko uhalisia.

tukirudi kwenye mada; jiulize ungekuwa wewe ni huyo bwana ugefanyaji au ungejisikiaje?

Anonymous said...

kamala kweli hilo ni igizo maana binti hana msutuko wowote,ila mimi ninashauri ukimfumania mkeo au mmeo lakini kwa vile mimi nimwana mme ngoja nisemee upande wangu,ukifumania ni bora mara mia ukasamehe au ukaacha watu wanawezakukuona mjinga au mwoga lakini ni bora ukasmehe maana hakuna asiyefanya hivi,na sio wakati wa ndoa hatakama ulitembea na msichana ujanani nikwamba ulishawahi kufanya zinaa ila mke wa mtu mtamu............we acha tu sijui kwa vile hamjazoeana!!!msinishangae