Thursday, January 19, 2012

NI MSIMU WA MAEMBE/NINA HAMU YA KULA EMBE!!

Nimekaa hapa nikawa nawaza kuwa sasa ni msimu wa maembe, mmhhh nikapata hamu. Natamani kweli embe. Maana msimu huu huwa maembe yanakuwa mengi mpaka wengine wanalisha nguruwe...Je wewe una tamani matunda gani? au chakula gani?


8 comments:

sam mbogo said...

Yasinta kweli msimu wa maembe, maembe haya yana mjina yake,mfano embe dodo sifa yake kuu nikufananishwa namziwa yanayo tamanisha ya mwanamke.utasikia wakisema duh!! toto ziwa dodo.
pia embe za kunyonya,embe hizi nividogo dogo vitamu sana,aina nyingine niembe bolibo sasa iliembe kwakweli silijuwi vizuri natoa mji anaye lijuwa. halafu picha hii mbona wauza maembe wote vigoli ndo wana kuwa hivyo baadaye watasimulia utoto wao ulivyokuwa.kaka s.

SIMON KITURURU said...

Mie umenitamanisha EMBE!

Baraka Chibiriti said...

Mimi kama wewe Dada Yasinta.....huwa nakula maembe kwa siku hata 50, napenda sana tena sanaaaaa tu!

EDNA said...

Mmmmh mie udenda unanitoka.

SIMON KITURURU said...

Samahani: Nahamu kweli ya embe ila embe jingine . Je Si EMBE ukitaka unaweza kuligeuza maana?

Nachokoza tu Kapulya hasa kama umewahi kustukia EMBE laweza kuwa sio EMBE!:-)

Yasinta Ngonyani said...

kaka Sam!mlinganisho huu umeniacha hoi, maana nilikuwa najua tu hayo majina lakini si maana yake..ahsante kwa hilo:-)

Mtakatifu! nimekutamanisha EMBE, ni kwasababu hizo ni embe au?

Kaka Bara embe hata 50 kwa siku au? Basi ww mwisho.

Edna! Sio peke yako:-)
Simon Kwani kuna embe nyingine zaidi ya embe?

ray njau said...

Raha ya embe ikutane na wali wa nazi ndugu zangu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray!! itabidi nikutembelee siku moja maana sidhani maishani mwangu nimewahi kula wali wa nazi na embe.