Monday, January 16, 2012

KUTHUBUTU KUONYESHA MAPENZI/UPENDO=MAISHA

Kuthubutu kuonyesha upendo wako,

sio tu maneno mazuri,

Na sio tu upendo wa matendo

Au maua na chokleti.

Ni kuonyeshana heshima,

uaminifu na imani.

Kuonyesha wepesi wa kuona huruma wakati mwanzako anapokuwa na

msongo/matatizo.

Kuwa msaidizi mwema na mwenye kusema ukweli.

Kuthubutu kuonyesha masikitiko yako,

Sio kila wakati kujifanya mwenye nguvu (mvumilivu),

Tukae/kaeni pamoja, tuthubutu kuwa watoto ndani yetu.

Tuwe sisi (Kuweni ninyi) kwa dakika chache.

Tuwe na dakika chache za furaha.

Tuwe na dakika chache za huzuni.

Tufanye siku iwe ya shangwe.

Tushirikiane katika raha na taabu katika maisha.

Tuwe waaminifu, tukaribiane na tupeane joto.

6 comments:

sam mbogo said...

Kinacho changanya nikujuwa yapi nima penzi ya kweli, kama haya ya kiulaya,kila baada ya dakika unmbusu mumeo/mkeo au yale ya kikwetu yanayo endasambamba na umambli( kwamba kumbusu mumeo/mkeo mbele ya kadamnasi si adabu njema,nk. je sisi waswahili mapenzi yetu yako ndani zaidi na wala si nje,kama wenzetu wa ulaya(weupe) mtoa mada umekamatia wapi unapo sema kuthubutu,nikupi huko kuthubutu,ni kama nilivyo toa mifano hapo ju au?.kaka s.

Goodman Manyanya Phiri said...

Yataka moyo!

chib said...

Somo hili... hakyanani halina kanuni! I mean, there is no formula!!

ray njau said...

Hapa ni vigezo na masharti ya maadili kuzingatia vinginevyo fomula itabadilika.
KUTHUBUTU + MAPENZI-UPENDO =MAISHA HATARISHI.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

achana navyo vyoote

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni sana wote kwa ushauri na hsa kwa kupita hapa .