Friday, January 27, 2012

PICHA YA WIKI ILIYOPENDWA NA PIA KUCHAGULIWA NA KIBARAZA HIKI !!

Inapendeza kuona watoto wanashika vitabu na kujifunza/kusoma. Sijui hapa anauliza mama/baba hii ni nini au wenzangu mnasemaje?

2 comments:

Mbele said...

Ni picha nzuri sana. Niliwahi kuandika makala nikielezea kuwa watoto wanapenda vitabu ila jamii huwaharibu wanavyozidi kukua. Soma hapa.

ray njau said...

Hii picha inawasilisha rasmi maudhui ya kibara hiki nahisi kichwa kisomeke:"HUU NDIYO MWANZO WA MAISHA NA MAFANIKIO YA BINADAMU"
-----------------------------------
Huu ndiyo mwanzo wa maisha na mafanikio kwa mtoto huyu anaonyesha hamu ya kujua kusoma,kuhesabu na kuandika ambao ndiyo mtaji wa maisha na mafanikio kwa kila mwanadamu.
-----------------------------------
CHANGAMOTO KWA WAZAZI NA WALEZI:
---------------------------------
Kutokana na ukuzi katika tasnia ya TEKNOHAMA inakuwa vigumu sana kwa wazazi na watoto kuketi pamoja na kubadilishana uzoefu katika tasnia ya elimu,mafunzo na stadi za maisha.Televisheni,intaneti na simu za viganjani ndiyo walezi wa watoto wetu.
----------------------------------
Mshuko wa maadili unaozidi kushika kasi katika ncha zote za dunia ni matokeo ya wazazi na asasi za kidini kuhamishia majukumu yao kwenye mikono isiyo salama chini ya falsafa na itikadi zisizo na mashiko.