Monday, January 9, 2012

HUU NI MLO WANGU WA MCHANA WA LEO KARIBUNI NI SUPU YA KAROTI!!


HAPA NI KAROTI AMBAZO TAYARI ZIMEMENYWA KWA AJILI YA SUPU
Karoti 6-8 kubwa,
Vitunguu 2
Vitunguu swaumu/saumu vipande 3,
Kijiko 1 cha siagi,
Vijiko 2 vya tangawizi iliyokunwa.
Lita 1 ya maji.
Vikombe 2 vya cream,
Vikombe 2 vya maziwa,
Kijiko1 chumvi
Pilipili kidogo/kadili upendavyo.
Jinsi ya kufanya:-
Menya karoti, vitunguu na vitunguu saumu/swaumu. Kisha kata vipande vipande. Yeyusha siagi na kaanga kwa dakika 3-5 kwenye sufuria kubwa. Weka tangawizi , kisha tia maji. Pika supu kwa joto la chini huku umefunika hadi karoti ziwe laini. Weka cream, maziwa na pilipili. Kisha unamixa na blender ya mkono mpaka kuwa laini. unawezawa kuongeza maji au maziwa kama unaona supu ni nzito. KILA LA KHERI NA UPISHI HUU:-)


15 comments:

Baraka Chibiriti said...

Asante sana, mi nitakuja kweli...shauri yako, halafu utaanza
kusema ooh ni kidogo, ha ha ha haaaa!!!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

niko njiani!

sam mbogo said...

naweka mafuta ungo wangu, ili niruke salama,usimalize supu. naomba nikute na kamkate kidogo.
kaka s.

Unknown said...

Mmmh recipes poa hizi dada... ngoja nami nitajaribu. Ahsante kwa maarifa na mlo mwema

chib said...

Utamu wa supu, uikute mezani!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka zangu :- Baraka, Chacha, Sam, Mrope na Chib wote mnakaribishwa sana na wala msiwe na shaka kuwa kweli tutashiba supu ipo tena nyingi tu. Karibuni sana tujumuike maana hapo ndo chakula kinanoga muwapo wengi...pia karibuni wengine wote

sam mbogo said...

Nilikuwa nikonjiani, na ungo wangu,ila nahisi kunambaya wangu mahali,nimeanguka naungo.naona aibu sitafika jinsi nilivyokuwa nimevaa,sasa sijuwi huyu atakuwa ninani....... au mgoni,msambaa, hapana sijuwi!! haya sikunyingine. kaka s

Goodman Manyanya Phiri said...

Hii sasa ndio tiba ya manjano kimlo au? Keroti zimezidi!! (LOL!!!)

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam, labda uliweka mafuta kidogo:-) ila sio mbaya siku nyingine, lakini siku nyingine jaribu kuchukua usafiri mwingine ili kuepuka huyo mshindani wako...

Kaka mkubwa Phiri! ndio maana inaitwa supu ya karoti. Ungeonja usingeacha kula kila wiki...

Rafikio wa Hiari said...

Rafiki asante kwa recipe hii nitajaribu week end hii halafu nitakujulisha kama imenoga hahahah!

ISSACK CHE JIAH said...

mimi jana nilikuwa nipo kwenye miahangiko jumapili nitainywa tuu kwa raha zangu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tazama naja upesi

ray njau said...

Ukarimu wa kingoni tumeukubali na tunakuja kwenye mlo huo ila msosi wenyewe ni kiduchu na ubahili.

Yasinta Ngonyani said...

Rafiki wangu wa hiari! yaani hutajigamba na nasubiri kwa hamu kunijulisha ilikuwaje:-)

kaka ISSACK CHE JIAH! nafurahi kusikia nijulishe baada ya kuinywa:-)

Kamala! mbona unachelewa upo wapi??? karibu sanaaaaaaaaaaaaa

Kaka Ray! Ahsante sana kwa niaba ya wangoni wote. Na wala usiwe na shaka kuna lisufuria lizima kwa hiyo hakuna ubahili hapa.KARIBUNI WOOOOTE

Anonymous said...

Maji ya kisima changu hayanyweki