Friday, December 30, 2016

FAMILIA YA AKINA NGONYANI IMEPATWA NA MSIBA ....BINTI PHILOMENA HATUNAYE TENA

Majira ya saa nne leo binti yetu Philomena Ngonyani katuacha baada ya kuumwa kwa  kipindi kirefu. Tunamwomba eeehh Mwenyezi Mungu atutie nguvu katika kipindi hiki chote kigumu.
Nitakukumbuka daima Shangazi yangu,

13 comments:

Evarist Chahali said...

Poleni sana kwa msiba. Philomena ametutangulia tu, sie sote tupo njia moja. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Evarist Chahali said...

Poleni sana kwa msiba. Philomena ametutangulia tu, sie sote tupo njia moja. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Evarist! Ahsante sana kwa pole na pia kwa kutupa matumaini kwa kipindi hiki kigumu. Amina.

Prince Emac said...

Daah! polen sana wapendwa kiukweli hakuna anaejua dakika inayofuata atakua ktk hali gani, sote tuu wake na kwake tutarejea...tuzidi kujiweka tayari kwa saa hiyo maana kila nafsi itaionja mauti...dada yetu katangulia nasi tunafatia ee mwenyez mungu mpokee mja wako

Yasinta Ngonyani said...

Prince Emac...Amina. Twasukuru kwa kuwa nasi katika msiba wa binti Philomena.

Anonymous said...

Poleni sana wanafamilia ya Ngonyani. Mungu azidi kuwatia nguvu katika hali mnayopitia sasa.

Nicky Mwangoka said...

Poleni sana Dada na Familia yote ya Ngoyani. Mungu awape wepesi kipindi hiki kigumu. Naungana nanyi kumwombea Da Philomena apumzike kwa Mungu palipo pema daima.

NN Mhango said...

Mungu awatie nguvu na kuwafariji. Hii ni safari ya kila mmoja. Kinachogomba ni kwamba hatujui saa wala siku.

Anonymous said...

Poleni Sana Kwa msiba wa binti yenu Philomena, Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Amin na awape wepesi Inshaallah. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

AHSANTE WOTE KWA KUWA NASI WANAFAMILIA ...KWA TAARIFA NI KWAMBA MAZISHI NI KESHO JUMATATU.

Mbele said...

Poleni sana. Mungu awape ustahumilivu na amweke ndugu yenu katika raha ya milele. Amina.

Ayubu Chewale said...

Goodbye friend.... RIP philomena

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu Mbele... Ahsante sana kwa kuwa nasi kwa kipindi hiki kigumu...

Ayubu Ahsante!