Saturday, October 23, 2010

Sweden:- Kwanini iwe hivi?


MUUAJI ATINGISHA JIJI LA MALMÖ NCHINI SWEDEN

Kuna mlenga shabaha anae washuti wahamiaji wanaoshi nchini Sweden Katika jiji la Malmö. Mlenga shabah huyo hatari anachagua wageni tuu ndio anaowapiga risasi.

Mpaka sasa idadi ya waliolengwa imefikia 15 ndani ya siku tatu..
Hali imezikuwa kuwa tata na wasiwasi sio kwa wageni tuu hata Polisi vichwa vinawauma maana mpaka sasa hawajapata muelekeo maalum ukoje.

Katika Mkoa wa Skåne ndiko kilipo chama cha wasiopenda na wana idadi kubwa sana ya wanachama wao kuliko miji mingine ya Sweden..Kwa habari zaidi soma Aftonbladet.se
habari kutoka blog ya kaka Michuzi
Mdau wa Iceland.
Nami ngoja niongezee hapa:- Tunamwomba Mwenyezi Mungu mauaji yasizidi kutokea kwani sasa kila mtu ambaye si raia wa Sweden anaogopa hata kwenda nje, dukani hospital hata kupeleka watoto chekechea na hata kwenda kazini ni woga sana. Kwa kweli hili ni jambo la masikitiko sana na wengi wanajiuliza kwa nini? Pamoja Daima.

10 comments:

Mija Shija Sayi said...

Yasinta mwenzetu uko mkoa gani? aisee haya mambo yasikilie mbali tu, poleni sana lakini huyo mtu au watu hawana siku nyingi watakamatwa, polisi wa wenzetu si masihara.

Yasinta Ngonyani said...

Mija Mie nipo mbali kidogo ila watu hawa wanatembea huko na huku. Mimi naishi Mkoa wa Värmland. Mzidi kutuombea.

emu-three said...

Oh twashukuru kwa taarifa hii, twawaombea mungu awalinde nyie mliokaribu na huko!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

zenofobia ya afrika kusini imihamia huko? duh! poleni!

tuko pamoja

Anonymous said...

...Hali imezikuwa kuwa tata na...

...Katika Mkoa wa Skåne ndiko kilipo chama cha wasiopenda na wana idadi kubwa sana....

...habari kutoka blog ya kaka Michuzi Mdau wa Iceland....

I HATE TYPOS AND CARELESSNESS...IT SAYS A LOT ABOUT THE PERSON...

Anonymous said...

hata mimi huku bongo najitayarisha kuwalenga wachina na mafisadi niombeeni nifanikiwe kuwaondosha nchini kwetu

Bennet said...

Poleni sana, hii niliiona kwenye taarifa ya habari ya aljazeera, hali ni tata mpaka wageni wanatembea kwa wasiwasi sana

PASSION4FASHION.TZ said...

Poleni sana,du! na hizi rangi zetu ambazo hata ukijichanganya katikati ya umati wa watu bado utajulikana tu wewe wa kuja,mungu atawaepusha jamani poleni sana.

Yasinta Ngonyani said...

hsante wote kwa maombi yenu na tuzidi kuombeana ili hili janga liishe na pia huyo mtu/watu wakamatwa na wawe panapotakiwa.Ahsanteni sana na mjadala unaweza kuendelea.

NAJUA WAJUA said...

Ni habari ya kusikitisha sana kwani ni mwanzo wa ubaguzi mpya duniani!

Poleni sana, mungu yupo nasi!