Tuesday, October 5, 2010

Tusisahau! Misemo na metheli toka Tanzania kwa lugha mbalimbali!!

1. Kibena:- Atembea na moto mgongoni.
Maana ya methali hii ni kwamba kama wewe si mkarimu, basi ujitegemee mwenyewe kwa kila kitu popote utakapokwenda. Methali hii hutumika kwa fundisho kwamba hakuna myu anayeweza kutenda jambo bila msaada wa wenzake. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

2. Kisukuma:- Fahamu kazi, usifahamu ngoma.
Maana ya methali hii ni kwamba ni vizuri kufahamu mambo ya maana kuliko kufahamu mambo yasiyo na maana. Hatumika katika kumwasa mtu ambaye anaanza kuzurura ovyo badala ya kyfanya kazi kama kulima, kusoma n.k.

3. Kiiraqw;. Haraka na pupa huzaa chongo.
Methali hii inaonya juu ya kukosa uvumilivu. Mambo mengi yafanywayo kwa pupa hayatimiziki na pia huleta matokeo mabaya. Methali hii ni kama ile ya kiswahili "Haraka haraka haina baraka"

4. Kisambaa:- Iliyonona huanzia miguuni.
Maana yake ni kwamba mtu mwema hujulikana haraka. Hutumika hasa katika mashauri ya kuchagua watu kwa shughuli fulani au kijana ayeleta posa, adabu zake na anavyofanya siku za kwanza.

5. Kipare:- Kabla hujamwua ndege usiwashe moto.
Maana ya methali hii ni sawa na ile isemayo:-
Usishone mbeleko kabla mtoto hajazaliwa. Asili ya maana ya methali hii hutokana na tabia za watoto za kuwinda ndege kwa pinde na mishale. Wakishamwua ndege humbanika na kumla. Jambo ambali linahitaji maandalio ya moto. Matumizi ya methali hii ni kuwaonya watu ambao wamezoea kupanga mipango juu ya mambo ambayo hayana uhakila asilimia kuwa yatatokea zaidi hutumika kwa mambo yanayohusu mali na ukwasi na mipango yako.

5 comments:

EDNA said...

Mbona umetusahau wanyalukolo?
Sisi tunasema: NIANGUSEGE TU.Hahahaha nakutania.

Yasinta Ngonyani said...

Mwanalukolo wala sijakusahao haraka haraka haina baraka. Siku yetu itakuja we kuwa na subira....

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

...ati niangusege...lol! Hiyo kali ha ha haaa!

Hii misemo bombi sana.. aksante kwa kutikumbusha!

Simon Kitururu said...

@EDNA: :-)

malkiory said...

Yasinta: Asante kwa kutukumbusha,methali hizi ni hazina kwetu katika harakati zetu za kujifunza kublogu.

Hii inayonihusu ya Kiiraqw ya kutofanya mambo kwa haraka haraka imenigusa. Nitazingatia kama mafundisho haya kwa njia ya methali toka kwa mababu zetu yanavyosema.