Tuesday, November 25, 2008

NI NINI KINAFANYA MAISHA YAWE NA FURAHA?

Hakuna kitu kitakacho weza kufanya maisha ya yako/yangu kuwa na furaha kama hatutakubali kujipokea mwenyewe na kupanga mfumo mzima wa maisha yetu. Wengi tunajikuta katika mahangaiko na mafarakano katika uhusiano iwe wa ndoa, au marafiki wa kawaida. Je? ume/tumesha wahi kukaa chini na kujadili kwa nini hili litokee, na je ni kweli kwamba katika haya yote hakuna jibu kwa matatizo haya.

Mpenzi msomaji katika kuchunguza hilo nimegundua kwamba tulio wengi hatuipi nafasi mioyo yetu kuchagua kile kilicho halali kwa matakwa yetu. Bali tunafuata mwelekeo wa mapendeleo yetu na tunaacha nafasi muhimu ya moyo kuupa nafasi ya kuchagua kilicho cha thamani zaidi ya furaha ya siku moja, ambao tuluo wengi tumekuwa tukililia au kuionea fahari. Hapa nina maana kwamba kama mwanamke ameahidiwa kuolewa basi atataka haja hiyo itekelezwe wakati hana uhakika wa kweli kama mpenzi wake anampenda kwa dhati.

Kuna misemo isemayo kwamba:- mwanamke anapotoa uamuzi wa kuolewa anafanya hivi akitegemea kwamba mwanamume anayeolewa naye atabadilika baada ya wao kuwa mke na mume; poleni sana wanawake tumepotea, dadili mwelekeo olewa na mtu mwenye mapenzi ya dhati na ambaye yupo tayari kutoa dhamiri yake kwa ajili yako.

Na kwa upande mwingine, Mwanamume anamwoa mwanamke na kumleta ndani ya nyumba akitegemea kuwa hatabadilika; Mungu ndiye ajuaye kuwa mwandamu ni kigeugeu, sasa atutendee nini ndipo tulidhike? Naamini wanawake wengi wanavumilia katika mahusiano ila wapo ambao nao ni wasumbufu, kwa sababu tu ya tamaa, na wengine hujikuta wanabadilika kwa kuwa maisha ni magumu ndani ya ndoa, na wengine umaskini, wanataka kupata chochote au kuiga ufahali wa wengine.

Swali linakuja je? unafikiri kukamatana ugoni na kuonyeshana kwenye vyombo vya habari kwamba nataka kumshikisha adabu ajifunze ni njia sahihi ya kutatua matatizo katika jamii kama watu hawata tumia njia ya kuiweka wazi mioyo yao kwa kile wanacho kipenda na kukitamani?

Ni changamoto kwamba kweli tulichokiamua pamoja na kukubaliana basi kiheshimiwe na kuthaminiwa kama kweli humpendi mwenzako sema tangu mwanzo liwe wazi tusitake maisha ya mtelemko kwa kuwa unayemwoa ana nafasi nzuri na wewe unavimba kichwa kwa sifa ya kazi yake na sio mapenzi ya kweli. Wewe utakuwa msaliti.

Maisha ya ndoa ni kuwa tayari kwa ajili ya mwingine wakati wa raha na shida, kwa furaha na amani bila majuto.

2 comments:

Unknown said...

Yasinta,
Ahsante kwa makala nzuri.
Changamoto inayowakabili wanaadamu ni kuishi na kufikiri kwa mazoea.
Sisi tunahangaika kwa sababu ya kuuridhisha mwili, walevi wazinzi na wezi wote wanataka kuiridhisha miili yao.
Ukija kwa wale matapeli wa mapenzi nao kwa tamaa huwatapeli wanawake kwa kisingizio cha kuwaoa wakati hata hawana upendo wa kweli katika nafsi zao kwa sababu ya kutaka kuifurahisha miili yao.
Sisi tumekuwa miili yetu inaendeshwa na utashi na si uhitaji.
Hatujiulizi kwa nini tunataka kufanya ngono, hatujiulizi kwa nini kutaka kulewa, hatujiulizi kwa nini tunataka kuiba,hatujiulizi kwa nini tunataka kudhulumu hatujiulizi kwa nini tunataka kutembea na wake za wa watu, kila linalotujia katika mawazo yetu ya kawaida tunataka kulitekeleza, bila kuupa mwili wa akili kutafakari na kutoa jibu sahihi. tumekuwa tunaendeshwa
na mwili na si mwili wa akili ambao unaweza kutafakari na kutoa jibu muafaka.
Yupo mtaalamu mmoja aliwahi kusema kuwa, kama wanaadamu wangeupa mwili wa akili nafasi japo kidogo ili uweze kujiridhisha kabla ya kuchukuwa uamuzi wowote, basi dunia hii ingekuwa na amani.
Lakini kutokana na kufikiri kwetu vibaya tumebaki kusingizia ibilisi, pale tunapopata matokeo hasi kutokana na matendo yetu.
jamani tujitambue.

Nitembelee www.kaluse.blogspot.com
karibu tujitambue.

Shabani Kaluse

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana kwa maoni mazuri Shabani na karibu sana tena na tena.