Monday, November 3, 2008

JE? MATATIZO NI KAWAIDA KATIKA MAISHA?

Matatizo, Matatizo kila kitu ninachofanya ni tatizo. Hata pumzi ninayotoa ni tatizo. Hata yule/wale ninaye/ninaowapenda ni tatizo.

Mwenzenu naumia, ninalia matatizo. Oh, matatizo matatizo. hata wale ninaowajali hawajali. Hata wale ninaowapenda hawanipendi niambieni nielewe ni kwa nini mimi, ninalia. Matatizo, matatizo.

Ni matatizo ya kila siku lakini yangu ni mazito niambieni nifanyeje ili niondoe matatizo haya. Maana kila kukicha ni matatizo, ni matatizo ni matatizo.

3 comments:

Unknown said...

Kwanza matatizo ni mazuri kwani hukufanya uwe mbunifu.
Pili huwezi kukwepa matatizo kama unaishi hapa duniani.
matatizo ni sehemu ya maisha tatizo kubwa linakuja jinsi unavyoliona tatizo, ukiliangalia tatizo tofauti basi tatizo huwa kubwa zaidi na ukiliangalia tatizo kama sehemu ya ufumbuzi au ubunifu au hamasa ya kufanikiwa na kupiga hatua basi ukipata tatizo badala ya kulalamika na kuona unaonewa utachangamka na kuanza kushughulikia.
Nahisi matatizo yangu ninayokutana nayo ni makubwa kuliko yako ila naamini yangu ni size yangu na nikiyashinda tu nitakuwa mbali zaidi na nitakuwa mtu wa mafanikio.

Ubarikiwe

MARKUS MPANGALA said...

matatizo nayo huwa yanazalisha stress sana kwahiyo laaima uwe imara kuyatatua lakini siyo matatizo ambayo yanakufanya uumie huku wanaokuumiza hawana chembe ya haki ya kukuumiza angalia usianguke

Yasinta Ngonyani said...

Asante Lazarus nitajaribu kufuata ushauri wako.Pole nawe kama una matatizo kama mimi

Markus nawe asante unayosema ni kweli kwani nimeona dalili. pia nadhani sitaanguka nitajaribu kuyafuatilia. karibu tena