Tuesday, December 9, 2008

NDOTO YA KUWA MTAWA/SISTA=MAISHA


Naona wengi mnataka kujua kwa nini sijakamilisha ndoto yangu ya kuwa mtawa/sista. Nitajaribu kuwaelezea:- Ni kwamba, nilikuwa na miaka 5-6. Nilikuwa nikiwaona masista nilikuwa naona kama wao ndio malaika nacheza nao. Nilikuwa nawaona wao ni watakatifu sana kwani muda wao wote waliutumia kusali tu. Ndio maana nikawa nawaza nami nitakapo kuwa mkubwa nitakuwa sista. Lakini sikumwambia mtu, Ni nini nakiwaza. Labda nilifanya kosa, kwani leo ningekuwa sista mwenzenu. Nikimtumikia mungu.
Habari ndio hii ndugu zanguni!!! Je? nimejieleza sawasawa?

13 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Umeniwahi maana nilikuwa napanga kukuuliza kilichotokea mpaka ukaacha ndoto yako ya kuwa sista. Na swali jingine ni kuwa wengi wasiokuwa masista huangukia kwenye unesi. Ni mavazi, ama wito ama kipi kinachoshabihiana katika "maisha" haya mawili ya usista na unesi?

Yasinta Ngonyani said...

Haya mzee wa changamota, Nitajaribu kukujibu kama mimi ninavyojua Usista unafanya kazi ya kumtumikia mungu na kila siku unaonana na watu. Na unesi pia unawahudumia watu na unaonana na watu wa aina mbalimbali na watu. sijui kama umeridhika na jibu langu.

Unknown said...

Nimesoma majibu yako, lakini bado sijaona kama umejibu swali letu.
naona kama umezunguka mno!!!!
Samahani kwa kuwa mdadisi,kwani rafiki zangu huwa wananiita Thomaso yule wa Biblia.
bado nasubiri Jibu.

Yasinta Ngonyani said...

Kama ni udadisi basi tumekutana. Lakini pia samahani hujaeleza ni kipengele gani sijajieleza kutosha.ukiniambia labda nitajaribu. kazi kwelikweli

MARKUS MPANGALA said...

imebaki kuwa ndoto siyo kweli. mimi niliacha kwasababu ya udadisi kwamba kwanini kuwepo na padre? lakini kweli kwanini uliamua kuacha kitu ukipendacho halafu ukawa nesi? mmmm sijui naona mada imenishinda dadangu
kwaheriiiiiii

Yasinta Ngonyani said...

Jamani vipi hii ni kama kumuuliza mtoto mdogo utakuwa nani utakapokuwa mkubwa. anajibu polis, kwa hiyo hapo si lazima atakuwa polis ile ni wakati ule tu anawaza vile lakini baadaye anaamua kufanya kitu kingine. VIPI sasa mbona hivyo.

Unknown said...

Nami nijitokeze kusaidia kujibu swali labda, naamini mtu anapoamua kuwa sista anakuwa amejitoa zaidi ya kawaida kwamba mwilim wangu utamtumikia Mungu maisha yangu yote kiasi kwamba wengine hatuwezi, Pia kama si kuwa sista akiwa nesi hujitoa (wito) kutumika zaidi ya mshahara ambao huliwa kwani kumsaidia mgonjwa ni zaidi ya mshahara, ndiyo maana binafsi nikisikia nesi amegoma huwa najua huyo hana wito wa kuwa nesi bali amejiajiri kuwa nesi kupata kipato au mkate na si wito kwani nesi wa kweli hawezi kuacha mgonjwa afe sababu ya kucheleweshewa mshahara.
Unesi au usista vyote ni kujitoa na zaidi kuwa na sauti ndani ambayo huwafanya hajsikie raha na furaha kuifanya hiyo kazi ndo maana wengine tunaona ni ngumu.

Hayo ni mawazo yangu tu!

Upendo daima!

Unknown said...

Ahsante sana kwa majibu yako,
Nilitaka tu kujua sababu ya wewe kutotimiza ndoto yako.
awali nilidhani kuwa labda ilitokana na shinikizo la wazazi.
Kwani wapo baadhi ya wazazi wakisikia mtoto wao anataka kuwa Padri au Sista wanakataa kwa hofu ya kukosa wajukuu.
Lakini kwa upande wako kumbe haikuwa hivyo.
Nakutakia mafanikio mema kwa shughuli zako za kila siku.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ok, ok, mavazi meupe yanavutia saaana ehe?
lakini mimi nadhani kuna mechi unazoijoy bila kuwa sisita na usingezifaidi kama ungekuwa sisita.

mahayafai kuwa siri.

Fadhy Mtanga said...

Mmh, mi sisemi kitu. Tangu lini? Nasema kitu, oh no, nauliza kitu, hiyo ndoto, I mean huo usista siku hizi hauufeel? Tatizo sijui kuuliza maswali vizuri, namaanisha huhisi kukosa kitu kwa kutokuwa sista?

Rama Msangi said...

Huwa ni ngumu sana kwa dunia ya sasa kila mtu kutimiza ndoto zake hasa zinapokuwa za kuwa MTAWA wa namna yoyote ile. Maana unapokuwa mdogo unakuwa na dreams zako, wazazi wanatakiwa kujua what are your dreams, ila hatuna utamaduni wa kuwaambia ili watupe miongozo ya namna ya kuzifikia ndoto zetu. sasa basi, amtokeo yake ni kuwa unapofikia rika lile wazungu wanaliita Foolish Age, unaamua kuonja tunda la kati na hapo unanogewa matokeo yake baadae unakujakuta he! kumbe nilishaharibu msingi wa ndoto yangu.

tatizo linakuwa wewe hukuwaeleza wazazi wako, pili wazazi wenyewe huenda wangeelezwa wasingekushauri maana hatuna utamaduni huo, tatu unatumbukia katika raha kuu ya dunia kwakuwa hujui hata ndoto yako inatamka nini kuhusu hilo.

Yasinta Ngonyani said...

La hasha kaka znguni kama ningewaeleza wazazi wangu wangeniunga mkono na sasa ningekuwa sista. Ila semani kama kaka msangi alivyosema hatuna utamaduni huo.

Rashid Mkwinda said...

Duu kazi kweli kweli,yaani Yasinta ulifikiria kabisa kwamba iko siku utakuwa Sista, hivi nikweli ungemudu misuosuko ya kilimwengu katika duani hii iliyosheheni matukio ya kidhambi dhambi?mie naamini huwezi kuwa mtawa ilhali bado unaishi kwa matamanio nadhani wale waliofikisha umri wa kutokuwa na matamanio kabisa ndio wenye fursa ya kuwa watumishi watawa wa nyumba ya MUNGU.