Thursday, December 11, 2008

HIVI NDIYO MWISHO?

Leo nimeamua kuandika hivi kwani kila asubuhi nikiamka ni giza na niandapo kulala ni giza na hata nitembeapo ni giza:-

Pake yangu barabarani natembea,
Kuna mtu anakuja nyuma yangu,
Je? naweza kugeuka na kumwangalia nyuma?
Peke yangu katika njia hii na gizani
Peke yangu - hakuna aliye nami.

Kwa nini lazima nitembee peke yangu?
Wakati nataka tuwe wengi?
Nipo peke yangu gizani, bila penzi,
Na mtu wa kunituliza. Kwa nini?

6 comments:

Unknown said...

Du! peke yako, bila mpenzi?
Pole sana dada.....
lakini angalia nyuma kuna simba Luwala.

Unknown said...

Mhhh!!

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta sikujua kuwa u mshairi mzuri kiasi hiki.
Umeandika vizuri sana kiushairi. Nimeipenda.
Lakini upweke si jambo zuri kwa binadamu.
Binadamu anahitaji faraja, anahitaji mtu wa kumtuliza, mtu wa kumliwaza.
Peke yake, binadamu huiona dunia chungu na maisha yanaboa.
Umeandika vizuri sana. Bado naitafakari tungo yako.
Alamsiki.

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni wote, Shabani simba hali watu bwana.

na hapo Bongo Pixs hiyo Mhhh sijaelewa.

Fadhy pia shukrani najaribu kuandika na napenda sana shairi. ila wote hilo shairi haliniusu mimi msije akadhani ni upweke. kazi kwelikweli

MARKUS MPANGALA said...

jamani mapenzi ni nini?
napata wazimu miye
kwani mlopatana mnafanyaje?
kupenda ni kazi ati usambe utajiri maana haya mambo bwana. LAKINI hakuna mwisho dadangu siamini hilo kwani unapotembea hauko peke yako amini kuna mtu karibu yako, anakujali na kukuthamini zaidi yao, ni mwema kuliko wema wenyewe. hayuko mbali geuka mtazame, angalia kwa umakini anakuja pembeni yako. hakika utapata faraja kwani aliyejuu mfuate juu ahina maana kumngojea chini. hata kinyozi anapunguza bei baada ya kuona ugumu. Hakuna mwisho penzi linagli moyoni mwako, unalo linahitaji ulione kwanza au halina mwenyewe? hapana hakuna mwisho bali ni changamoto moto za hapa na pale. anayekupenda hasemi mengi ni mkimya,mtulivu,mstahimilivu hata akikamatwa na F.F.U hakuna noma kwani hana fujo bali hutulia na kuamua anachokipenda. Mwangalie tena, umemuona huyo hapo?

Unknown said...

Ni vijimambo dada, ni pale utamanipo kusema na usijue usemeni hasa. ndo twaishia Mhhhh.