Monday, December 8, 2008

MAPENDO NI KITU GANI?:-INAENDELEA

Mifano ya upendo wa kweli

Kuna mifano mingi ya upendo wa kweli katka maisha ya kila siku. Kuna upendo wa baba unaojihakikisha kwa kumpeleka mtoto wake mgonjwa hospitalini. Baba anapaswa kutembea porini maili kumi na tano bado baada ya safari ndefu, lakini baba anasukumwa na upendo, anapata nguvu na ananuia kufika hospitalini. Wala hawezi kusema, “Inatosha sifanya zaidi ya hapa.”

Kuna pia upendo wa mama ambaye kila siku huleta faraja, nguvu na kitulizo kwa watoto wake.

Upendo wataka kukua

Upendo ni kama uzima. Wote tunajua ya kwamba mungu ndiyo chanzo cha uzima wote. Uzima, unaishi, unakua na kubadilika. Hivi ndivyo upendo ulivyo. Ni lazima utiririke na kukua. Ni budi uenee, utafute maeneo na mahali papya pa kusitawisha na kutajirisha. Upendo upo kwenye matengenezo wakati wote. Tunajua upo, lakini kila mara unahitaji kufanywa upya na kukua. Kama sivyo upendo unakufa.

Ufanyacho upendo

Upendo kidogo ni kama jua, ambalo ni rafiki yetu wa daima. Hufukuza baridi, huimarisha mazao yetu na kuyaivisha. Hivyo ndiyo ufanyavyo upendo, kama jua. Katika kupendana, yule mwenye kupendwa hubadilika. Anabadilishwa kutoka hali ya mashaka, wasiwasi, hofu, upweke na kutoamini, anakuwa mtu mwingine kabisa. Mwanzoni alikuwa mwenye hofu na mashaka, sasa ni mwenye kujiamini na kuthubutu kutenda. Badala ya uchungu na upweke, imekuwa furaha na heri. Ni kama nyoka abadilishaye ngozi yake ya zamani kwa wakati fulani, na kubaki na ngozi mpya. Kwa upendo aliopata mtu huyu amafanywa kuwa mpya.

Mara nyingi twasikia watu wakisema, “Huyu mvulana anampendaje msichana huyu?” au , “nini cha kuvutia alichonacho Bwana huyu?” Haina maana kuuliza kwa nini twampenda mtu mwingine. Kama ni mapendo kweli,hatumpendi mtu kwa kuwa ana vitu fulani vya kuvutia wala hatumpendi ingawa ana kasoro, bali tunampenda mtu aliye ndani ya yote haya.

Upendo: fumbo la ajabu

Kama nilivyosema juu ya upendo kuwa ni kutoa nafsi yako. Hii bado haielezi kikamilifu maana ya upendo. Kwani upendo ni fumbo la ajabu. Ni fumbo kwa sababu maana yake ni nzito mno hata kika siku tunajifunza kitu zaidi juu yake.

Na kwa kweli, tunaweza kupata maana kamili ya upendo kutoka kwa Mungu peke yake ambaye Neno lake latuambia:-
Upendo huvumulia, hufadhili,
Upendo hauhususu,
Upendo hautabakari, haujivuni
Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake,
Hauoni uchungu, hauhesabu mabaya
Haufurahi udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli,
Upendo huvumulia yote, huamini yote, hutumaini yote na husatahimili yote.

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

Upendo ni wa ajabu, nguvu kushinda mauti,
Thamani ya dhahabu, kwa wenye kismati,
Ukiwa naye muhibu, mambo mengine hufati,
Upendo huleta raha.

Upendo ni mfariji, pale uwapo shidani,
Hata uwe muhitaji, utajihisi una amani,
Muumba ndiye mpaji, upendo wenye thamani,
Upendo huleta raha.

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy kila siku unaweza kumfanya mtu awe na furaha. Lao umenifanya mimi niwe na furaha. Asante kwa kipende hiki cha shairi I love it.

Fadhy Mtanga said...

Nimepata furaha sana kwa kuwa umefurahi. Kazi yako ni nzuri sana. Blog yako ni moja ya zile blog makini.
Ahsante sana kwa kukipenda kipande hicho.
Alamsiki.

MARKUS MPANGALA said...

sawa huwezi kuhesabu mabaya!! jamani mimi naamini katika falsfa hii UKIONA MTU HANA KAWAIDA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU BASI HAJUI AENDAKO WALA AKIFANYACHO, sawa kweli unapenda sana lakini lazima kupayuka wakati mwingine tena kwa domokali sana hata kama unaupendo namna gani. Mbona Yesu aliwapayukia wale waliovamia hekalu na kuweka biashara zao?
mmmmm nimeshindwa, umeshinda dadangu haya chukua tano za hewanii hiyaaaaa mazeyaaaaa

Yasinta Ngonyani said...

ASante Markus, ila mimi hapa nilikuwa na nia ya kubadilishana mawazo! ni hilo tu