Saturday, December 27, 2008

BLOG MAISHA SAFARINI = YASINTA


Blog Maisha, nimeona ni vema niage sitakuwa hewani kwa muda kidogo NASAFIRI. Nakwenda Peramiho, nakwenda ungonini. Nakwenda kula likolo la nanyungu na malombi (mahindi ya kuchoma) Wangoni wote myumwike?
Walongo Vangu!!!!
Tutaonana karibuni tena. KWA HERINI KWA MUDA. NAWATAKIENI WOOOOTEEE MWAKA MPYA 2009.

13 comments:

Anonymous said...

Tiyumwike, kwali wamuyitu, karibu panyumba. Tikuganila safari njema, vasalimilahi voha kunyumba, paruhuwiku, kuperamihu, kuluhagala, kulitumba, kuchingoli, kotukayi kukosiwa kuhuluka palipokela kuvajambusa valongo vangu. wihamba kunyumba wakati kamsimu ka kulima nde kayingili, magela mtindu umonga kuni, likolo la nanyungu lakona ndava fula yicheliwi kutonya, malombi nde kabisa, gakona sana, kwanza kwali ngati yati tilima sana namwaka ndava, mbolela yikweli behi sana, eti mfuku umonga shilingi elufu sitini kwali ngati yati tilama namwaka. lakini majibu tipewili, yatilima sana mayahu, ena apu tikitahi kyani ngati mbolela kawaka pala? ukahuma huko tokukayi kukosewa kunigegela kangowani (ulelema, urundi, na ngowani mgunda), halafu chigoma na udagala wa kunyanja, chonde dadangu yangu, nauli ya kunitumila kuhuma kuswideni yati nikupela, nene yati nilindila hapa pa paris, au wijova wuli dada? yitikilayi basi!!

ngalilihina

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta, wala usingetuaga, unakuja nyumbani. Unakuja kwa baba na mama. Unakuja, unakuja. Karibu sana.
Hatupendi kusikia unaacha kublog hata kama ni kwa wiki moja. Wanakijiji hatupo radhi kuambiwa kisima chetu kinakauka hata kama ni kwa siku chache.
Hatutafurahi. Usipumzike kublog, mawazo yako yanahitajika sana.
Lakini kokote kule uendako, tafadhali usiache kutukumbuka katika sala zako. Tuombee daima.
Karibu nyumbani, lakini katika mtandao tutakumiss, hatutamani iwe hivyo.
Kila la kheri!

Anonymous said...

Tena kwa kuungana na Fadhy Mtanga, napenda kumkumbusha dada Yasinta kwamba hata akiwa Songea anaweza kublog, kuna vijiwe vya internet kibao Songea mjini, kimoja wapo kinaitwa Valongo, kipo katika jengo la mabruda wa Hanga, linatazamana na soko kuu la Songea mjini pale jirani na NBC, ndio kusema toka Ruhuwiko kuja mjini sio mbali, pale ni dala dala, shilingi mia mbili (sijui kama imepanda hiyo nauli kwa sasa), hivyo anaweza kuja mjini haraka kutupa habari, tena sasa hivi tunazisubiri za moto moto za kilimo, na ulanzi. changamka dada, hatupo tayari kuvumilia kwa muda hata kama ni wiki moja, pambwani hapa dada tunzayi wateja vaku, upiliki?

Fadhy Mtanga said...

Kweli kabisa. Kama Songea kuna internet cafe kwanini tunyimwe changamoto mpya za maisha? Hapana, hatuna uvumilivu huo. Hatuwezi.
Sisi si watu tuuonao umuhimu wako katika kutokuwepo kwako. Sisi si tu tunauona umuhimu wako, ama tunautambua, bali tunauona, kuutambua na kuuthamini.
Blog yako imesheheni changamoto za ukweli za maisha.
Tafadhali usiache kublog, ndilo niwezalo kulisema.
Ahsante sana!

MARKUS MPANGALA said...

Samahani naomba kumsahihisha huyu asiyejulikana hapo juu kwamba kuna mgahawa wa mdalakilishi pale jirani na soko kuu unaitwa Valongo. Lakini nijuavyo mgahawa ule unaitwa SONGEA NETWORK CENTER ndiyo unaotazamana na soko kuu, kuna nyingine nayo ina kasi nzuri ila wahudumu VIMEO{wabovu} sana ipo karibu na ofisi za chama cha CCM {CHAI,CHAPATI, MAHARAGE}. Nakuhakikishia kwamba SONGEA NETWORK iko bomba na inapakana na benki ya NMB siyo NBC?? nadhani umenielewa sasa au vipi mwanawane. Ukija Mbinga ipo ambayo napenda utulivu na kasi yake inaitwa LOTIKAA CAFE ipo mtaa wa Frastoo ukitoka maktaba ya wilaya pale kuelekea kaskazini mashariki mwa hoteli ya Savanna. Labda hii Valongo siijui ni ngeni au mimi sijui. PIA najua unakuja na Laptop yako kwahiyo labda ukajibidishe kulima hapo nitakuelewa mkuu au vipi mlongo.

LAKINI karibu nyumbani dadangu mwenga yaani nikunogili kweli mbno uchelewa sana bambu veve mmm henu safari kukingoli au Ruhuwiko? Lundo je? shangazi yupo pale au? karibu nyumbani tena.

Anonymous said...

Asante kwa masahihisho ndugu Markus. Ni kwamba hiyo unayoisema Songea Network Center itakuwa ni hiyo hiyo, kwani mimi nina muda mrefu kidogo sijarudi kusalimia Songea, ilipofunguliwa hiyo internet ilikuwa inaitwa hivyo Valongo(ilifunguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge 2002 au 2003 kama sijasahau sana hapo), labda sasa hivi imebadilishwa jina, ila nakumbuka sana hilo jina Valongo, na kama ulivyosema kwamba pia ipo jirani na NMB. Ujirani wa kitu unategemea unataka kusema kwa mtazamo gani, mimi nilitumia NBC kama reference frame yangu kwa vile nayo pia ipo karibu na hilo jengo, nilitumia NBC kwa vile ni benk kongwe hapo Songea na kila mtu ukimuuliza inakuwa rahisi kuijua na kutoa maelekezo. Unajua katika utaalam wa jiolojia wanasema huwa tunatumia reference majengo au vitu ambavyo kila mtu anakifahamu kwa urahisi, sasa kwa kipindi chote ambacho mimi nimekuwa Songea hilo jengo la NMB halikuwa na umaarufu wa kuweza kutumia kama reference frame japokuwa nafahamu kwamba nalo lipo karibu na hilo jengo ilipo hiyo internet cafe. Lakini cha msingi ni kwamba ujumbe umeeleweka na imefahamika inapopatikana hiyo cafe, by the way hiyo cafe nawafahamu mpaka wamiliki, wahudumu, na kadhalika kwa vile nilikuwa mteja wa kudumu sana nilipokuwa hapo nyumbani kwetu.
Asante tena bwana Markus, mnyasa wewe!!!

Sharuvembo Hill said...

Safari njema, Mungu akulinde usafiri salama wewe na familia na zaidi ufanikiwa kwa yale yote unaenda kufanya.
Tutakumiss sana.

Upendo daima

Mzee wa Changamoto said...

Nadhani ndio MAISHA hayo. Sina la kuongeza zaidi ya kukutakia Kila la kheri katika safari.Tutakuwa sote kwenye hisia na maombi

Unknown said...

Haya na mimi, naona niseme, nisalimia huko uendako.
Ila kama wadau wengine walivyosema kwamba hata Songea kuna vijiwe vya kublog, basi ukutuhabarisha mawili matatu yatayojiri huko, naamini yako mengi.
Mimi nasubiri nyepesinyepesi za huko.

John Mwaipopo said...

karibu tanzania, karibu songea.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

kila jema katika safari ya kuelekea NYANDA ZA JUU KUSINI..kama sijakosea jiografia ya nyumbani.

Nimependa jinsi ulivyo mwaga huo mstari ambao mara ya mwisho niliusikia akiunena Dr Remmy kwenye kibao chake anarudi nyumbani...

Wasalimie LUKURUFUSI,Ruhuwiko,maji maji,mfaranyaki,seed farm..

wasalimie LIZABANI..mi nina shahuku kubwa sana ya kuona picha ya lizaboni na DELUXE HOTEL..NIMEMISS SANA SONGEA..

KILA JEMA..TUPO PAMOJA

Christian Bwaya said...

Karibu nyumbani dada yetu. Ila usiache kublogu

Anonymous said...

häjjj... lätt å fatta vad som står, tänkte ta en titt härpå ditt äventyr men vi talar inte samma språk :o) från anonym på parkvägen