Wednesday, December 17, 2008

MAISHA YA ENZI ZA KIKOLONI (UTUMWA)

Wazungu walitutesa sana. Huyo kijana alichukuliwa toka Afrika na kupelekwa Marekani kuwa mtumwa. Je? hii ni haki kweli?

18 comments:

Christian Bwaya said...

Kuna wenzetu wanaofikiri ni haki. Ndiyo maana hwaishi kutuona kuwa tu watumwa wao. Tu watumwa sisi. Tumefungwa japo twajiona tu huru.

Unknown said...

NAOGOPA KUSEMA.

Simon Kitururu said...

Tukumbuke kuwa watu weusi tulikuwa pia tunauzana hata kabla ya utumwa kuongezewa kasi na waarabu na wazungu. Mpaka leo hii Ndani ya Afrika hasa Afrika ya kati, magharibi na kaskazini utumwa unaendelea.Kuna nchi kama ghana ambako tukusifiako bado kuna maeneo watu wana watumwa.

Unafikiri auae zeruzeru kwa ajili ya kidole anashindwa KUWA NA MOYO wa kumuuza Simon Kitururu kwa matumizi ya kumuogesha mke wake?:-(

Anonymous said...

Nakunukuu "Huyo kijana alichukuliwa toka Afrika na kupelekwa Afrika kuwa mtumwa"
hapo sijakupata, ninavyofahamu mimi huyo kijana anapatikana katika filamu (series) ya "roots au racine kwa kifaransa", anaitwa Kunta Kinte katika filamu wakoloni walimbatiza Tobi, alichukuliwa Afrika kupelekwa Marekani na sio Afrika kupelekwa Afrika.

Yasinta Ngonyani said...

Bwaya nimekuelewa ni kweli tu watumwa bado mpaka leo.

Shabani kwa nini unaogopa kusema kuwa huru ndugu yangu.

Simon nakubalina nawe lakini pia nadhani bila ya wazungu kuanzisha huo utumwa kweli tungekuwa watumwa kwa sisi wenyewe?

Na wewe usiye na jina nimekupata na sawa kabisa tayari nimebadili. Asante.
Na pia asanteni wote.

Unknown said...

YASINTA,
NILIOGOPA KUSEMA KWA WASI WASI KWAMBA NITACHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA BLOG HII AMBAYO NI KISIWA CHA TAALUMA.
NADHANI MAONI YANGU YATAWAUDHI BAADHI YA WATU.
KAMA UNASISITIZA NITATOA MAWAZO YANGU KESHO ALFAJIRI.

Yasinta Ngonyani said...

Toa tu maoni yako huu ni wakati UHURU kama kweli tuna UHURU.Asante

MARKUS MPANGALA said...

jamani Yasinta anajua misimamo yangu kuhusu hawa jamaa waliojifanya kueneza neno la mungu huku wanasema nendeni kwa amani utumwani. ngoja nitarudi kwa AYA za moto labda mnikataze. nilikuwa nawaslimia tu leo nitatoa maoni machweo kesho alhamis

Fadhy Mtanga said...

Hivi binadamu ni nani? Wana hisia gani wanapowauza binadamu wenzao mithili ya bidhaa?
Wamemwasi Mungu hao. Wanahitilafu vichwani mwao.
Ok, walimwasi Mungu, walikuwa na hitilafu vichwani mwao.
Nimeeleweka.
Alamsiki!

Anonymous said...

Simon, umewakilisha mawazo yangu haswa... utumwa sio tu uarabuni au uingereza au amerika.... ukoloni na utumwa mambo leo...neo-colonism imezidi.

Jasinta...asante kwa kutuletea blogu inayochemsha bongo...nendelea hivyo hivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Serina karibu sana tena sana hapa kijijini. Na asante kwa mchango wako!!

Unknown said...

Yasinta,
Uhuru wa kutoa maoni ni lazima pia usitumike kuwaumiza wengine kihisia.
Nilikuwa najaribu kutafakari kuhusu utumwa wa kiakili ambao ndio tulio nao leo.
Kwani utumwa wa akina KUNTA KINTE, Kwangu ni kama mzoga uliokwishaoza.
sihitaji kuukumbuka tena kwa sababu nitaumiza hisia zangu bure na kujenga chuki kwa kile kizazi cha wale walioleta yale madhila.

Yasinta, utumwa wa kiakili unatutesa mpaka leo.
wale waliojipa mamlaka ya kufikiria badala yetu wametusaliti mchana kweupe.
Wamejiongozea mamlaka zaidi na sasa wanauza kila kilicho mbele yao.
Maandiko matakatifu yalitumika kutupotosha ili kukubaliana na maamuzi yao.
hao hao waliotuuza utumwani wanarudi kwa kasi ya ajabu, wakitumia mbinu mpya ya utandawazi.

Hivi sasa kila mtu ameamua kuwa mjanja.

Naomba msije nirushia mawe.

Hivi dada Yasinta, unafahamu kuwa, njia rahisi ya kuwakamua masikini hapa nchini ni kuanzisha kanisa.
Kila mtu amamua kujenga kanisa lake ili kuwatawala watu kiakili, kwa kutumia maandiko matakatifu.
Wamegundua kuwa watu wamekata tamaa, na ukitaka kuwapata kirahisi wahubirie neno la mungu ambalo halina tija kwao, zaidi ya wao kunufaika.
Hapa ndipo tunaposhuhudia aliyenacho kuongezewa.

Hebu tembea uone jinsi wananchi wanavyokamuliwa na fungu la kumi.
Kila kukicha watu wanazindua nyumba za ibada utadhani ni hizi albam za bongo fleva.

Inauma sana tena sana, kukuta mtu mzima na akili zake anakubali kudanganywa hivi hivi!!!!!!!
Tunahitaji kujikomboa kutokana na utumwa huu.
Yasinta nina mengi ya kusema lakini naomba niishia hapa, ili niwape wengine nao nafasi ya kuchangia.
Niliahidi kukutembelea leo alfajiri.

Karibu kibarazani kwangu ujitambue,
kwani sijakuona siku nyingi.

Yasinta Ngonyani said...

Shabani haya yote usemayo ni kweli kabisa. Na hii ndiyo sababu ya kuweka hii picha kwa nina uchungu sana kwa sababu mtu huwezi kumfunga mtu mnyororo kama mbwa, kwani hata mbwa wenyewe wako huru.asante sana kwa maoni yako.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta kinachokupa uchungu nini ni? inamaana bila hiyo picha kupigwa usingepata uchungu?

biblia inasema, enyi watumwa watiini mabwana zenu. kwahiyo kukomesha utumwa ni kuenenda kinyume na neno takatifu la mungu ktk biblia, Amen

Mzee wa Changamoto said...

Luta. Unapingana ama kuungana na neno ulilonukuu? Kuna mifano huwa unaitoa kama inapingana ama yaonesha una wasiwasi na maandiko na kwingine ni kama unayatumia kwenda tofauti na wachangiaji wengine. Ninapata shaka kujua kama lengo ni kuwa tofauti na wachangiaji ili kuleta changamoto ama vipi? Ni namna nionavyo tatizo na naamini yaweza kuwa ndio tatizo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mzee wa changamoto sidhani kama umekosea, uko sawa kabisa, tunawalaumu wengine huku tukiwakubatia. tunakuwa kama mtoto aliyebebwa na mamae harafu anampiga. tunaamini biblia harafu tunapinga maelekezo yake. tunachukia utumwa wakati biblia inatuwambia tuwe watumwa. wapi na wapi.

!

Vimax Pills said...

nice pos and article, thanks

Meizitang Botanical said...

i like it this blog, thanks