Sunday, December 21, 2008

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA

Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.

Na pia nakuomba:

Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA

8 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana da Yasinta kwa kutukumbuka na kututakia Jumapili njema. Nami naungana nawe kuwatakia ndugu zetu Jumapili njema.
Tukumbuke kuwaombea wale wenye uhitaji, wanaosumbuliwa na maradhi, njaa, kunyanyaswa na kadhia zote.
Pia tuwaombee wale wenye ujasiri wa kunyanyasa wengine, kudhulumu wengine, kuwaumiza wengine. Wale wenye ujasiri wa kuzungumza wakijawa na nyuso za tabasamu huku wakitambua kuwa kuna watu wanaumia ilhali wao hawajatimiza wajibu wao kuzuia hayo.
Tuombe kuhusu mambo mengi sana. Lakini kubwa zaidi tuombee amani na furaha na matumaini na upendo mioyoni mwa watu wote. Tuombe ili dunia pawe pahala salama.
Tuombeane tuyashinde mapungufu yetu.
Amina.

Unknown said...

Ahsante kwa sala nzuri,
Jumapili ya leo imekuwa si nzuri sana kwangu, juzi nilikuwa mwezeshaji kwenye mjadala fulani wa kitaaluma.
Kutokana na kuongea kwa muda mrefu koo langu limepata mushkeli na hivyo kuniletea homa.
Hata hivyo baada ya kusoma Sala yako nimepata nafuu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kaluse unamaanisha ungesoma sala hii kabla ya kuingia kwenye mjadala huo, koo lisingeuma?

da yasinta kwa nn tumwombe bikra maria na ni kwanini anaitwa bikra japo alizalishwa? sio bikra tena huyu!

Anonymous said...

Usengwili sana Yasinta, sala ya bwina sana, Domika ya lelu nipatili amani ya mahele sana, ndava ya sala yaku. Ujovili chakaka sana timuwombaya mahu Bikira Maria atiwombelahi kwa mwana waki, wasalimilahi wajomba vangu kutali huko.

Ngalilihina.

Mzee wa Changamoto said...

Asante Da Yasinta kwa kutuombea na kututakia siku njema. Nawe pia uwe na wakati mzuri na wale wenye taabu a mihangaiko pia wawezeshwe kulingana na imani zao.
Kila la kheri kwa wote na mwanzo mwema wa wiki ijayo.
Blessings

Unknown said...

DU NILIKUWA SIJAONA, KUMBE UMEWEKA PICHA NYINGINE!!
UMEPENDEZAAAA!!!!!!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy, shabani, kamala, mzee wa changamoto na wewe usiye na jina asanteni sana kwa maoni yeni.

Shabani asante kwa kuipenda picha yangu hiyo nimepiga jana.

MARKUS MPANGALA said...

aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah acheni hizo na MIMI nisiye na jumapili mwana wa afrika nifanyeje. mmmm nimegundua kitu KWAHERIIIIIIIIII