Friday, December 26, 2008

SALA YA FAMILIA PAMOJA

Napenda kuwashukuru wana-blog wote kwa ushirikiano mzuri mlionao. Kwa hiyo leo nimeamua kuweka sala hii kwani pia kumshukuru mungu kwa yote nawaombeni kila mmoja kwa nafasi yake na wakati wake aiombee familia yake kabla mwaka huu 2008 haujaisha kwa sala hii asanteani sana:

Milango imefungwa, Ee Bwana.
Yule mtoto mchanga amelala.
Tunajisikia salama., tuna raha ya ndani, kwani tumeshiba.
Chakula kilikuwa kizuri, kinatuletea faraja.

Huu ndio wakati wa kukugeukia.
Mwisho mwa siku hii ya leo, kama familia – familia yako,
Ambapo Kristu anaishi.

Kwa ajili yetu, kila mmoja wetu; Bwana tunakushukuru.
Kwa ajili ya siku hii ya leo, iliyojaa mambo mengi,
Mema na yasiyo mema sana, Kwa yote tunakushukuru.

Tunapoangalia nyuma, mara ngingine, ni rahisi kuona,
Kwamba ingeliwazekana kuwa vizuri zaidi.
Hapa na pale, tumeshindwa kukupendeza. Kwa neno la hasira,
Na lile ambalo hatukulitimiza.

Tunasikitika, Bwana tusamehe. Kwani tunahitaji upendo wako.
Tunakuhitaji wewe, ukae nasi usiku huu wa leo,
Ili kutulinda, kutubariki. Kwani wewe ndiwe kuta za kweli na paa za nyumba hii.

Utubariki tulalapo. Utujalie ndoto zetu ziwe za furaha.
Na utujalie tuamke kesho. Tukiwa na uzima mpya tele.
Nguvu mpya na starehe mpya, ili tuweze kuishi tena siku nyingine.

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta, ahsante sana kwa kututhamini. Mungu akubariki sana.

Unknown said...

Aaamin, mungu akubariki katika shughuli zako.
Ahsante kwa sala nzuri.

Koero Mkundi said...

Dada Yasinta, naomba unifundishe kuomba, mimi kila siku nagombana na mama yangu, kwa sababu siwezi kuomba.
Inaonekana mwenzangu we mzoefu wa maombi.
Kila siku mama yangu huniambia kwamba kama sitaomba basi sitafanikiwa katika maisha, lakini mbona nilifaulu na kujiunga na chuo? au ni kwa sababu najiamini?

Fita Lutonja said...

Haya asante rikizo njema dada Yasinta, wasalimie wote wanaonijua na wasionijua pia wape hai waambia nimewamisi