Wednesday, December 24, 2008

MFANO WA WAWILI WALIOOANA: ”STEFANO NA MARGARET”

Soma hapa na utoe maoni yake;-

Margaret na Stefano walikuwa wameadhimisha harusi yao miezi miwili iliyopita. Ilikuwa sikukuu kubwa. Marafiki wote wa Margaret, wanaofanya kazi ya uganga, na wafanyakazi wa idara ya kilimo ammbako Stefano anafanya kazi, wote walikuwepo. Miezi miwili imepita tangu sikukuu ile. Tangu zamani Stefano na Margaret walikuwa wanafikiri kwamba wanafahamiana. Wakati wa miezi sita ya uchumba walikuwa wamewahi kuzungumza mara chache kwa dhat juu ya mambo fulani. Lakini mara chache tu. Sasa matatizo yalianza kutokea, kwa kweli matatizo mengi.

Siku moja, Margaret alimwuliza Stefano, Ni aina gani ya chakula unataka ninunue kwa majuma mawwili yajayo? Bila kujali Stefano alijinu; Nunua chochote kile upendacho. Margaret alimtazama na mara Stefano alikwisha toka nje. Siku iliyofuata alimwuuliza tena, Stefano, unaonaje ikiwa tutanunua cherehan, naweza kujishonea nguo zangu? Bila saburi Stefano alijibu, Unafikiri nitapata wapi fedha zote hizo? Hakuwahi kuchukua muda kidogo na kukaa na Margaret ili waone pamoja kama kwa miezi ijayo wangeweza kufanya mpango wa kuweka akiba ya kiasi fulani cha fedha na baada ya muda Margaret angeweza kujipatia cherehani.

Mwezi mmoja ulipita. Usiku mmoja Stefano aliporudi nyumbani alisema, wiki ijayo nitakuwa safarini. Unatambua jinsi anavyomjulisha Margaret juu ya uamuzi wake. Hakuongea juu ya msafara wake wala hakumshirikisha kwa nini alitaka kwenda.

Unafikiri Margaret alikuwa anawaza nini kichwani mwake? Usiku huo alikwenda kitandani na kuanza kufikiri. Stefano hanipendi wala hanijali. Nikimwuuliza juu ya kitu fulani haonyeshi kuwa kinamhusu hata kidogo. Nikisema nahitaji kitu fulani ananiambia hatuna fedha. Lakini sasa yeye atafanya safari na hiyo safari inahitaji fedha aliendelea kuwaza je kwanini anasafiri? Atakwenda na nani? Kwa muda gani atakuwa safarin? Ananiache peke yangu bila kujali jinsi ninavyojisikia. Sawa, nami nitafanya vivyo hivyo. Nitatunza mshahara wangu wa mwezi huu ninaopata toka hospitalini na nitakwenda nyumbani kwangu. Nitakaa huko kwa muda wote nitaopenda:- Swali:- je? Hapa kunakosekana nini?

4 comments:

Unknown said...

KITU KIKUBWA KABISA NA MUHIMU KINACHOKOSEKANA HAPA NI MAWASILIANO.
MAWASILIANO NDIO MHIMILI MKUBWA KWA WANANDOA.
KWANI KWA KAWAIDA MAWASILIANO YANPOKUWEPO KWA WANANDOA UPENDO UTAFUATA WENYEWE.
KWA HIYO YANAPOKOSEKANA MAWASILIANO KWA WANANDOA BASI NA NDOA HIYO JUA KWAMBA IKO MASHAKANI.

Simon Kitururu said...

Hawa jamaa wanaongea kama mwanamume na mwanamke.

Unaweza kukataa!

Wanawake na wanaume wanamsisitizo tofauti katika mambo mengi ambayo yapo yatakayoitwa muhimu.

Ushauri kwa wanaume kutoka kwa uzoefu wangu binafsi, msikilize mwanamke wako na fikiria asemacho mara mbili hata kwa ujifanyaye bingwa wa mawasiliano.

Fadhy Mtanga said...

Yap, nakubaliana na wakubwa hapo juu.
Mawasiliano jambo muhimu kuliko.
Pia naamini hawakupata muda wa kufahamiana vema kabla hawajaoana. Lakini pia nadhani kuna kutojiamini baina yao.
Ni hayo tu.

Christian Bwaya said...

Mwasiliano. Naambiwa mawasiliano yana hatua tatu. Moja mazungumzo ya matukio. Mbili mazungumzo ya watu wengine. Tatu na ndio mawasiliano yenyewe, mazungumzo ya kuhusisha hisia za wanaozungumza. Hawa sijui niwaweke kundi lipi.

Nadhani kuna haja ya watu kufahamiana vyema kabla ya kuoana. Hawa jamaa nadhani hawakuwa wanafahamiana vya kutosha.