Thursday, August 6, 2015

UJUMBE WA JIONI YA LEO TOKA KWANGU KUJA KWENU

Maisha  ni mtihani Mkubwa na tofauti. Watu wengi huwa wanafeli kwa sababu wanajaribu kuiga maisha ya wengine, bila kujua ya kwamba kila mmoja ana swali lake tofauti.

2 comments:

NN Mhango said...

Da Yasinta umepiga pabaya leo. Ni kweli upendo si vitu wala utimamu bali utu na thamani ambayo mhusika anayo. Nadhani huyu mzee alionyesha jinsi ambavyo mwenzake hakubadilika moyoni mwake pamoja na maafa yaliyomkuba. Nadhani tafsiri rahisi na kweli ni kuwa kile kiapo tunachokula kama kikiheshimiwa na kutolewa kwa ukweli, hata mwenzio awe vipi bado atakuwa na thamani. Nadhani hii inakwenda hata kwa wazazi. Wanapozeeka sana wakapoteza kumbukumbu na uwezo mwingine huwa hatuwasahau kwani tunajuwa wao ni nani katika maisha yetu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! ulichosema ni kweli kabisa nakubaliana nawe kwa namna fulani...Pia nafurahi sana kuwa na asili niliyo nayo.