Saturday, August 8, 2015

UJUMBE WA LEO

Ilikuwa ni majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo mzee mmoja mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 aliingia katika
hospitali moja ili kusafisha kidonda chake cha mguuni.
Mzee akaanza kwa kuomba afanyiwe haraka kwa kuwa alikuwa na appointiment
ya muhimu sana ifikapo saa tatu kamili ya asubuhi hivyo afanyiwe msaada wa
huduma ya haraka.
Daktari mmoja akaguswa na mzee yule baada ya kuona kila mara akiingalia saa yake na kutikisa kichwa cha kukatishwa tamaa na kuamua kumhudumia kwani alijua ingechukua zaidi ya saa kabla ya
mzee kuhudumiwa kutokana na idadi
kubwa ya watu kwa kuwa yeye hakuwa na
mgonjwa wa kumhudumia wakati huo.
Baada ya uchunguzi wa kidonda chake
kikaonyesha kuwa kimepona na daktari
akaanza kukifungua akishirikiana na nesi
kukisafisha. Wakiwa wanaendelea kukisafisha
kidonda daktari na mzee wakaanza mazungumzo na daktari akamuuliza kama mzee alikuwa na apolintiment na daktari mwingine kwa jinsi alivyokuwa na haraka.
Mzee akajibu hapana, ila natakiwa kuwahi kwenda kunywa chai na mke wangu
ambaye amelazwa kwenye kituo cha kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya ubongo .
Mzee akaendelea kumwambia daktari
kuwa mkewe amelazwa pale kwa zaidi ya
miaka miwili akitibiwa maradhi hayo na hana kumbukumbu kabisa
 Daktari akauliza sasa kama kapoteza kumbukumbu atakumbuka kama umechelewa?

Mzee akamjibu daktari kuwa mke wangu hajawahi kukumbuka kuwa mimi ni nani au nini kinaendelea kwa zaidi ya miaka hiyo miwili.
Kwa mshangao daktari akamuuliza, "Na umekuwa ukiendelea kwenda kunywa
naye chai kwa miaka yote hiyo kila siku asubuhi hata kama amekusahau wewe ni
nani?"
Mzee alitabasamu na kuushika mkono wa
daktari na kumwambia "hanifahamu tena
mimi, ila mimi bado namfahamu ni nani
kwangu na umuhimu wake kwangu"
Daktari alifuta machozi huku akimtazama
mzee yule akiondoka kulekea kwa mkewe
kunywa chai kabla ya saa tatu kamili.
Daktari alijishika mikono yake kichwani na kusema, "Hii ndio aina ya mapenzi
ninayoyataka katika maisha yangu"
Upendo wa kweli hauko kwenye mwonekano wa mtu au mapenzi. Mapenzi
ya kweli ni kukubaliana na hali zote zilizopo, zitakazotokea na ambazo
hazitatokea pia.
Kama umeguswa na kisa hiki tafadhali
CHANZO:- NIMETUMIWA NA RAFIKI

1 comment:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yasinta umepiga pabaya leo. Ni kweli upendo si vitu wala utimamu bali utu na thamani ambayo mhusika anayo. Nadhani huyu mzee alionyesha jinsi ambavyo mwenzake hakubadilika moyoni mwake pamoja na maafa yaliyomkuba. Nadhani tafsiri rahisi na kweli ni kuwa kile kiapo tunachokula kama kikiheshimiwa na kutolewa kwa ukweli, hata mwenzio awe vipi bado atakuwa na thamani. Nadhani hii inakwenda hata kwa wazazi. Wanapozeeka sana wakapoteza kumbukumbu na uwezo mwingine huwa hatuwasahau kwani tunajuwa wao ni nani katika maisha yetu.