Monday, August 17, 2015

KUMBUKUMBU:- LEO NI MIAKA KUMI NA MOJA (11) KAMILI TANGU MAMA YETU ALANA NGONYANI ATUTOKE!!

MAMA! ANAWEZA KUCHUKUA  NAFASI ZA WENGINE LAKINI NAFASI YAKE HAIWEZI KUCHUKULIWA NA YEYOTE YULE
 
KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka kumi na moja  sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana, sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!

5 comments:

NN Mhango said...

Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu mama yetu. Aaaamin

ray njau said...

Poleni sana ndugu zetu na endeleeni kudumisha mioyo iliyojengewa uvumilivu.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni sana kaka zangu kwa kuwa pamoja nasi kwa siku hiii ya kumbukumbu ya mama yetu.

Mama Wane said...

Poleni sana na Mungu amrehemu mama yetu.

Yasinta Ngonyani said...

Mama Wane! Kwa niaba ya familia ya Mzee Ngonyani nasema ahsante kwa kutufariji.