Tuesday, April 24, 2012

SWALI HILI LIMENIKERA SANA:- MAJINA YA SAMAKI YANATOKA WAPI???

HAPA NI SAMAKI AINA YA MAGEGE
Ni muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza kuhusu majina ya samaki. Juzijuzi nilikuwa nikiangalia habari/pragramu kuhusu ziwa Nyasa, ziwa Viktoria na Tanganyika. Nikakumbuka majina ya samaki kama vile :- Kambale, Mbofu, Mbelele/sengefu, Magege, Vitui, Vindogo, Mbasa nk. Nikawa najuiliza hivi ni maeneo ya ziwa nyasa tu tunawaita hawa samaki hivi au? Na kama ni hivi nani aliwapa samaki hawa haya majini? Sikupata jibu...nikaona niliweke hapa kibarazani  hili swali. Kama nisemavyo/nijuavyo palipo na wengi hapaharibiki kitu. Tuwe pamoja katika kamjadala haka

12 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

Dada leo inabidi ujibu maswali mengi hao ni changu kule pwani kule kwetu kweli ni magege na kule mwanza sijuwi ndo satoo au vipi wewe MBOGO MKWE WANGU ANAKUPIKIA MWANANGU RECHOEL UNASEMAJE?
TUPO PAMOJA
CHE JIAH

batamwa said...

Hayo majina yanatokana na sehemu lilikoziwa na majina mengine ni kutokana na kibantu kwa maana lugha zinategemeana,huko kwetu ziwa la Rwelu sisi tunawaita "Engege,kuna eningo,kuna enshonzi{kambale},enkorongo yenyemwiba mgongoni,emputa{sangala},na wengine nawengine............

sam mbogo said...

Ewe baba mkwe mpendwa,che Jiah. kama ulikuwepo binti yako anajuwa mapishi sana hasa ya samaki .mimi hupenda samaki anaitwa sato,bila kusahau kambale,nk. nikweli majina ya samaki yanategemea nasehemu wanapopatikana,na mazigira yake kwa ujumla,hasa walaji. Tena dada Yasinta si samaki tu kuna ndege majina yao mengi ni ya kiluga na ukifuatilia utajiuliza swali kama hilo hapo juu majina yao yanatoka wapi?. kaka s

nyahbingi worrior. said...

Amani.Mzima Dada,nimepita kukusalimu hapa kijiweni.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ceh Jiah! Nashukuru kwa mchango wako sikujua changu na magege ni samaki mmoja...

batamwa! ahsante nimejifunza lugha mpya hapa naona ninyi mnaanza kila mara na "N" ila hilo jina la ENKORONGO duh! kaazi kwelikweli..

Kaka Sam! Hakika ukiwa mdadisi na utajifunza mengi kwani haya yote tusingeyajua..Umenikumbusha ni kweli kuna majina ya ndege yaaaani basi tu umenikumbusha enzi hizo ufikapa msimu wa kulinda mpunga mweeeh!!!

Kaka nyahbingi worrior! Nashukuru kwa salamu ni kweli ulikuwa umeadimika kivyake..Karibu sana!!

Penina Simon said...

Teh teh teh!!!! na wewe Yasinta unawaza mbali jamani,
Mimi nadhani wavuvi au wale wanaouza samaki ndio hutoa hayo majina ili kurahisisha manunuzi kwa wateja wao, na kwa bidhaa walizo nazo.

ray njau said...

Watani zangu wapare hapa umewafikisha thame.

batamwa said...

dada Yasinta mhhh mbona "ENKORONGO" jina kama limekutatiza kidogo au lina maana nyingine kikunyumbi!

Yasinta Ngonyani said...

batamwa! ndiyo "enkorongo"lina maana nyingine kabisa na siwezi kusema hapa SAMAHANI.. hasa ukitoa hiyo "e"

batamwa said...

haya dada Yasinta hiyo ndio lugha gongana hiyo

Yasinta Ngonyani said...

kweli kabis ana naamini hili batamwa!!!

Rachel siwa Isaac said...

Tehtehtehte baba yangu che Jiah!!!!!che bwana wee Sam mwana wa Mbogo hahahaaha!!Mungu awabariki sana na wooote waliopita hapa!!
Ahsante dadake kwa kutuletea majina ya Chamaki!!!!