Friday, April 20, 2012

MZIKI NI MOJA YA BURUDANI KATIKA MAISHA....


Leo nimepumzika kubeba maboxi  na bahati mbaya huko nje kuna mvua na kaubaridi kwa hiyo nikawa niriwadhika kwa kikombe cha chai na mziki, na ndipo nikakutana na kipande hiki na nikaona ni vizuri niburudike nanyi....jioni njema kwa wengi na wengi sijui asubuhi, mchana au usiku?

8 comments:

sam mbogo said...

Hakika kweli usemayo Dada Yasinta Ngonyani,muziki nichakula cha roho! wengine wasema muziki ni sabuni....! pia kama usemavyo muziki ni burudani. kiafya muziki nitiba/dawa. asante kwa muziki huu usisahau kuucheza pia ili ukamilishe tiba.
kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

KakaSam! hahahaha...una mbwebwe wewe, haya muziki pia si mziki tu ni ujumbe pia na halafu uchezapo sio unacheza tu unapata na mazoezi.
Ahsante kwa misemo yako hapo juu ila sasa kucheza peke yangu huwa sipendi sana:-(

Anonymous said...

dada yansita pole na majukumu ya kutuhabarisha mimi niko uot of topick hivi dada uliona ule ujumbe wangu wa recipe ya chapati au hukupata muda dada natumaini ikipata muda mziri utanijibu tu maana wewe huwa muungwana sna ni hayo tu tuanshuku kwa blog yako nzuri ubarikiwe sana dada

ray njau said...

Muziki una uwezo wa kugusa papachi za moyo wa mwanadamu na kuamsha msisimko mwili mwake.
Wanazuoni wa sanaa na muziki wanauelezea 'country music' kuwa ni muziki wa kishamba ambao ulipigwa huko Marekani toka enzi za kale ukiwa na lengo la kuwahamasisha wafanyakazi wa mashambani wasahau maumivu yao ya kazi za shambani na kusonga mbele kwenye malengo ya waajiri wao.
Ukitaka kufahamu siri iliyojificha ndani ya muziki fuatana na Masoud Masoud wa TBC Taifa[Tanzania] akupe vionyo na ladha za kale ambazo kwa vijana wa sasa ni adimu kabisa.Enzi hizo utapewa mpango kazi kuanzia kwa watunzi,wapiga vyombo,watia sauti,waimbaji na mafundi mitambo.Lakini leo ni enzi za teknohama na wanasema'everything under one roof'.Hapa ni faida au hasara?

isaackin said...

dayasinta muziki na chai kweli hiyo safi sana maana unapata ujumbe,ukija kwangu ni muziki na john mtembezi,au vodka originale au mwalimu ndo muziki inanoga.nitembelee bana

Yasinta Ngonyani said...

usiye na jina hapo juu.Usikonde nipo mbini na hiyo recipe ya chapati..asante kwa kunikumbusha.

Kaka Ray! Hiyo au huo mziki ni wapi kutafuta. Maana mie na zamani ni marafiki sana.

Kaka Isaac! we acha tu chai na mziki ndo penyewe..huko kwa kjohn mtembezi na hiyo vodka ..swali la kizushi mwalimu kama mwalimu au maana yake nini? Usikonde ntakutembelea nawe karibu sana kwetu:-)

Ausal said...

Habari Yasinta!hongera kwa kuruhabarisha na kutuburudisha, nakupenda sana fkira zako na maisha yako kwa jumla, muziki huu naupenda sana na hasa hicho kipengele ulichokiweka ndio huwa kinanifurahisha sana! ila kilichonichanganya katika mziki huu ni pale Msechu anapoonekana anavunja mawe na huku mpenziwe anaishi ghorofani.

Rachel siwa Isaac said...

Ngoja nijaribu kuimba kidogo labda nitapata wa kuniingiza studio.
Mziki asili yake wapi eeh, Mziki ni wanani eehh,Usinione nikiimba ukazani nina furaha ,kumbe.......koh koh kohh kohh,Duhh hii fani imenishinda yaani Mungu chumba hiki alinisahau kuniingiza!!!!

Ngoja nicheze tuuu,Ahsante dadake kwa Muziki.