Tuesday, April 17, 2012

MAISHA: NAIPENDA MIKOBA YANGU NA NAZIPENDA SKAFU/SHALI ZANGU!!!

HAPA NI BAADHI YA MIKOBA NIIPENDAYO
HAPA NI BAADHI YA MIKOBA YANGU

NA HAPA NI SKAFU ZANGU
NA HAPA NI SKAFU ZANG
Katika maisha sisi binadamu tupo tofauti kwa kila namna. Tukianzia tabia, sura, mwili, kupenda nk. Leo napenda kuzungumzia neno KUPENDA/TAMAA. Lakini si kule kupenda kwa kimapenzi hapana ni kupenda kwa kupenda vitu au kupenda kununua vitu hata kama anavyo vya kutosha:- Yaani utakuta mtu anapenda kikombe chake cha chai kweli kiasi kwamba mwingine akikigusa ni balaa. Mwingine anapenda kweli shati moja tu ambalo anaweza kulivaa kila siku utazani hana lingine. Mwingine akawa anapenda sweta kiasi kwamba hata kulifua anasahau. Halafu kuna hawa wanaonununua viatu, utakuta mtu ana pea za viatu chumba kizima huwa nashangaa sana je atavivaa lini? lakini hii yote ni basi tu yaani tamaa . Na kuna wanaokusanya/nunua vitabu. Kwa hiyo leo nataka kuwaambia mimi ni MDHAIFU SANA wa SKAFU/SHALIna MIKOBA. Hapo juu ni zaidi ya ishirini na bado natamani zaidi kwani nataka niwenazo rangi zote. NAPENDA SANA SKAFU.....NA PIA MIKOBA Swali je wewe ni mpenzi/mkusanyaji wa nini?

8 comments:

ray njau said...

Hapa ni wanawake katika mchakato wa maisha na mafanikio yao.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray unataka kusema wewe hakuna hata kitu kimoja ambacho unakusanya au unapendelea kununu hata kama unacho?

ray njau said...

Duh;hili ni swali ndani ya swali.Acha nifikirie vizuri.

ngaizaskids said...

Hapa umegusa penyewe my sis, mimi ni viatu na mikoba yaani hapo nimekwisha. Juzi juzi hapa mr.kaniomba niwapunguzie Red Cross nikamwambia mimi siwezi anisaidie, na kweli akanisaidia sasa hata miezi miwili haijapita nimeshajaza pale alipotoa na kuzidisha mwee huu ugonjwa hauna mganga ati.

DOROTHY MARTIN NDUNGURU said...

mi napenda sana viatu. yani chumabni kwangu kuna viatu vingi kiasi kwamba vingine labda nishwahi kuvivaa mara moja au hata mara moja hadi badaye naishia kuvigawa. mikoba kwa kweli ndo ugonjwa wangu mkubwa. Tukija katika vyombo vya jikoni, napenda sana glass...yani kuna wakati najiona kabisa si mzima kwa jinsi ninavyopenda kifaa hiki!!!

Anonymous said...

hiyo kuwa na viatu au vitu vingi ambavyo huvitumii ni tamaa kama ya chui yeye kazi kuua wanyama anapandisha juu ya miti tai wanakuja wanachukua hivyo ni ugonjwa au sio ugonjwa ni uharibifu au ulafi maana ulafi sio kwenye chakula tu

EDINA J KIBOMA said...

Yasinta umenifundisha neno jipya la kiswahili leo..SHALI.
Mi pia napenda mikoba na ila sinunui mingi kiasi cha kushindwa kutumia yote,Kila nilichonacho ninakitumia.

Yasinta Ngonyani said...

Duh! nimefurahi kuina tupo wengi wenye tamaa. Ila kama mmoja alivyosema hapo ni uLAFI tu. Ni mara nyingi pia nimewaza hivyo lakini inakuwa kama mnywaji pombe asipokunywa basi ni shida tu...Ila kama tukikaa na kufikiri sana tungeweza kufanya kitu kingine cha maana zaidi...Nimefurahi Ngaizakids shemeji alivyoamua..hii safi sana .