Wednesday, April 4, 2012

JIONI NJEMA....MNAKUMBUKA WAKATI ULE JINSI WATU WALIVYOKUWA WAKIANDIAKIANA BARUA KAMA HIZI??

NIMEONA TUENDELEE NA JUMATANO HII YA MARUDIA NA HIII...KARIBUNI

Baby Hujambo
Nimekaa hapa mbele ya computer yangu usiku huu , nafikiria leo nikuandikie kwa lugha gani , ili uelewe ninachotaka kusema , mwanzo nilitaka kuandika kwa kiingereza lakini nikasema mhh inawezekana baadhi ya maneno matamu nikakosa bora niandika kwa lugha yetu takatifu Kiswahili Baby ni jambo la furaha sana kupata nafasi hii nyingine kukaa mbele ya computer kukuandikia kitu Fulani , kuna watu saa hizi wanalia wameumizwa na wapenzi wao kwa njia moja au nyingine , kuna wengine saa hizi wanafikiria kesho itakuwaje kwa sababu wamewauzi wapenzi wao , kuna wengine wameshakata tamaa ya maisha kwa sababu walijitoa sana kwa wapenzi wao mwishowe walikosa vyote walivyokuwa wanafikiria hapo mwanzo Pole kwa kuongelea mambo hayo hapo juu lakini ni kukumbusha tu wajibu wako katika kuhakikisha mapenzi yetu kati yangu na wewe yanadumu na kuendelea kukua siku hadi siku , kila siku unaposoma ujumbe wako ujue tu kwamba nimekufikiria kuliko jana kwahiyo nakupenda zaidi natamani uwe karibu yangu ili maneno ninayoandika nikuambie moja kwa moja , ili ujisikie maalumu zaidi . Pamoja na hayo mimi hapa nilipo naendelea vizuri sana , namshukuru mungu toka asubuhi mpaka sasa hivi umefika wakati wa kupumzika hakujatokea tatizo lolote zaidi ya moyo wangu kusikitika kwanini sikuwahi kukujua toka mwanzo nilipoanza kuwa na akili timamu nimeanza kukujua tu ukubwani , kwanini haya mapenzi ya sasa hivi sikuyapata huko kwingine kote ndio nakuja kuyapata sasa hivi ukubwani natamani ingekuwa hivyo toka mtoto mpaka sasa na hata ninapoaga dunia . Ahsante sana kwa mapenzi ya dhati unayonionyesha na kunipa kwa kweli naamini mimi ndio mwanaume bora kuliko wote duniani na tukiwa na familia basi ntakuwa baba bora kuliko wote duniani nikiwa na wewe , kwa jinsi tunavyoishi sasa hivi nina ndoto na malengo mazuri sana kuhusu wewe sijawahi kuwa na wasi wasi wowote mpaka sasa hivi . Baby naomba uendelee kuwa mwaminifu mvumilivu na mwenye malengo katika maisha yetu sote wawili , mie pia naahidi kuwa mwaminifu mvumilivu na malengo katika maisha yetu sote . Napenda kukuahidi kukupenda , kukujali na kuwa na wewe wakati wote wa maisha yangu toka uliponijua sintojutia kukupenda wala kuwaza lolote baya kuhusu wewe kama yalikwepo basi yafute anza maisha na mambo mapya katika maisha yetu sote wawili Nakupenda sana , naomba niishie hapa niende kupumzika sasa hivi Ha ha ha haaaaaaaaaaa…………………………sio mimi jamani……………………Kaaaazi kweli kweliHii nimeidesa Jamii Forum……………..

1 comment:

Anonymous said...

Mwandishi kakosea katika kufikisha ujmbe, kwanza enzi hizo matumizi ya kompyuta hayakuwepo, hivyo asingesema nimekaa mbele ya kompyuta yangu na pili neno baby halikuwa linatumika wakati ule vinginevyo maneno ni mazuri.