Wote tunakutakia kheri sana kwa siku hii maalum kwako kwa kutimiza miaka. Twakutakia mafanikio mema katika maisha na kila jambo ufanyalo pia familia yako . Kumbuka kwamba sisi ndugu, marafiki, wajombo, watoto, shemeji twakupenda sana. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA SAVIO.!!!!
Kwa vile leo pia ni Ijumaa basi ngoja tusherehekee siku yako kwa kipande hiki cha muziki:-)
19 comments:
Hongera kaka Sovio. Mungu akulinde na kukuongezea miaka zaidi.
Jamani yasinta mbona mwenzenu mmempa jina la kiitaliano...lol!
Da Mija sio mimi ila baba yetu alisoma na waitaliano na alinusurika kuwa Padre. Ndio maana tuna majina ya ajabuajabu:-)
Hongera sana braza Savio. Uwe na maisha marefu.
Da Yasinta sikufahamu umeongeza utamu jina la blog. We mkali. Limependeza.
Da Mija: hilo si la kiitaliano bali la KILATINI....lol
Da Yasinta: Alinusurikaje? nani alimnusuru?...lol
Swali zuri Chacha.
Ok, Samahani kwa kupindisha kiswahili kaka Chacha na Da mija ni kwamba alitaka kuwa padre lakini kwa bahati mbaya kulitokea kitu fulani ntamuuliza na nitawajibu ni kitu gani. Upendo Daima. Hongera kwa siku ya kuzaliwa Savio
Hongera kaka Savio....ujaaaliwe nguvu na miaka ya kuwaona wajukuu na vitukuu!
'ongela' ndugu savio. mungu akunyooshee mapito, upate miaka tele hata uone watoto wa wajukuu wako.
hongera kaka sovio hongera kwa siku yako ya kuzaliwa mungu aibariki familia yenu ma head phone ya nini dada Yasinta
umefana na kaka deo kweli dayasinta
kumbe ni style ya nyele mimi nilifikiri ni headphone lol
Usisahau kunywa ulanzi kidogo ukiwa umechanganya na pingu, ndo sherehe za kijadi. Hongera sana
du pingu!
YES! Lakini sherti afunge sarawili kwa chini ili spring na skrubu zitakapolegea awe ngangariii....lol
Hongera kaka Savio kwa kusherehekea siku yako ya kuzaliwa,
nakutakia maisha marefu
nje ya mada,:
eti mafanikio ninini?
Happy birthday Savio,Mungu akuongezee miaka mingi zaidi.
Happy Birthday Kaka Savio
kamala kufanikiwa ni wishes
wanting something to happen
I wish she will say yes
Mwaipopo: 'ongela' sio? napenda sana kiswahili chako.
Kwenu wadau: kwa kuzingatia maana hasa ya neno hongera, je tunapompa hongera mtu fulani kwa kufikisha miaka kadhaa, huwa tunamaanisha nini? Kuna alichofanya kuchangia idadi hiyo ya miaka au?
Post a Comment