Sunday, February 7, 2010

Jumapili hii ya sita ya mwaka tusali sala hii!!!!!!

Ee Mungu unifanya niwe chombo cha amani yako. Penye chuki nilete mapatano, penye kukata tamaa nilete matumaini, penye huzuni furaha, Amina

9 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Habari ya huko?

nilikuwa nimepotea sasa nimerudi tena.Natumaini wadau woote mu wazima.

Nimepita kuwajulia hali..

siku njema

wasalaam

edo

Koero Mkundi said...

Ngoja niendeleze.......
=Penye njaa tuletee shibe...
=Penye ukame tuletee Mvua..
=Penye kufeli tuletee kufaulu...
=Penye ugumba tuletee ujauzito..
=Penye giza tuletee nuru...
=Penye barabara za vumbi tuletee za Lami..
=Penye wagonjwa tuletee nafuu na uzima...
=Pasipo na kujitambua tuletee Utambuzi...
=Penye useja tuletee ndoa kama ya Kamala...
=Penye ujinga tuletee werevu...
=Penye maoni mbofu mbofu, tuletee MCHARUKOOO.......

=MWISHO NAWAOMBEA WALIOKO UGHAIBUNI WAREJEE NCHINI TUIJENGE NCHI WAKATI NDIO HUU NA KAMPENI ZIMEKWISHAANZA....LOL

Simon Kitururu said...

Ee Mungu unifanya niwe chombo cha amani yako. Penye chuki nilete mapatano, penye kukata tamaa nilete matumaini, penye huzuni furaha, Amina


Mungu wasaidie BINADAMu wakubali ubinadamu!

Kwenye chuki wakumbuke chuki ni msaada kwa binadamu kuwa binadamu.

Kwenye kukata tamaa wakubali ni kuachia wasio kata tamaa wapate ulaji kwa hilo na ndio UBINADAMU ambao ufanyao MATUMAINI yawe na maana.


Penye HUZUNI watu wahuzunike vizuri kwa kuwa ni ukichaa kwenye huzuni watu wasipokuwa na ufanisi wakuhuzunika.

Na labda wenye furaha WAINGIWE huzuni mara kwa mara KATIKA kuwasaidia wastukie ukichaa wa kuwa na furaha hasa katika dunia hii iliyojaa HUZUNI ambayo imegeuka ni ujanja kudharau yote mazuri yachangiwayo na HUZUNI.

Amen!:-(

NURU THE LIGHT said...

ahsante dada kwa sala...mbona kimya sana upooooo...ubarikiwe

Mija Shija Sayi said...

Nimegundua wote tungekuwa tukitafsiri maisha kama Mtakatifu Kitururu tusingekuwa na stress kabisa kabisa!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Amina!

Lulu said...

Ng'wanambiti hukufumba macho halafu umeitikia Amina!!!! Ahsante dada kwa sala nzuri. Tubarikiwe sote.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Lulu: Umijuaje kama sikufumba macho?

Na unadhani kuna tofauti kati ya kufumba na kutofumba macho wakati wa kusali? :-(

ama ndo habari ya kulia na kucheka zote ni kelele?

Baraka Mfunguo said...

Sala maarufu niipendayo ya Mtakatifu Fransisko wa Assisi.