Wednesday, February 24, 2010

Swali la leo :- Lahusu uumbaji+Meno kwa viumbe hai!!!

Mwenzenu nimeulizwa hili swali na watoto wangu niimeona ni vema kama nikipata msaada wenu kwani kwangu lilikuwa swali gumu kidogo. Swali lasema hivi:- Hivi kwa nini viumbe hai vyote vizaliwapo havina meno na baada ye huota meno? Na kwa mfano binadamu, baada ya kukua na kufikia miaka 4 mpaka labda 13 meno ya utatoni hutoka na kuota mapya. Na halafu jinsi wazeekavyo hupoteza meno yote. hivi ni kwanini?

13 comments:

John Mwaipopo said...

sio watoto wako tu, tupo wengi tunasubiri majibu hapa.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

MAPENGO wakati wa kuzaliwa na wakati wa kuzeeka: duh!

nadhani yanakuwapo kwa kuwa hayahitajiki wakati huo na yanapotea (meno kuota) wakati meno kuhitajika...lol

Mija Shija Sayi said...

Kijasho kimenitoka...

Itabidi tumtafute kaka Chib atupatie funguo ya chumba cha vilaza...lol

chib said...

@Da Mija: :-) Nilitaka kukwepa kujibu swali hili maana sikupenda sana kujulikana kama na mimi kwa swali hili naelekea kuwa kilaza :-)
Naanza kwa kusema uongo ufuatao
sio viumbe wote huanza kuishi bila meno, wanyama kama kobe na kasa huzaliwa na meno ambayo hayang'oki mpaka wafe labda ndo ukayang'oe(Mtadai kasa hazaliwi kwa sababu anatoka katika yai :-(
Mnyama mwingine anayezaliwa na meno ni hamster - Da Subi atatutafsiria hilo neno kwa kiswahili, mie nimesahau kidogo. Na huanza kutafuna moja kwa moja anapozaliwa, ndio maana wanamwita ya kuwa anazaliwa kula tu!
Kwenye mada sasa... nakuna kichwa kwanza, labda niulize swali tu
Kwa nini hususan binadamu mchanga na mzee kikongwe wanafanana japo kiasi katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na akili, maana kibabu anaweza kulilia pipi ati,..., umbo, meno aka kibogoyo, kazi, kuona, vyakula wanavyokula, maana sijamuona kijeba anatafuna mfupa.
Sorry nilikuwa najitahidi kukimbia ukilaza, natumaini mmenielewa

Bennet said...

Siku ukirudi ruhuwiko kawaangalie wale ndama ulioowaacha au wapigie simu jamaa zako, watakwambia kwamba mpaka na wao wameshazaa lakini bado hajaota meno ya mbele ya juu, sasa sijui kwa nini?
Ng'ombe huwa hawana meno ya juu ya mbele ila chini yako nane, na yale ya canine hawana juu na chini (kuna uwazi tu kama mapengo) halafu yanafuata premolars 12 (juu 6 na chini 6), na mwisho molars 12 (juu 6 na chini 6)jumla 32

EDWIN NDAKI (EDO) said...

swali nzuri..da mija msifunge mlango wa Vilaza tafwadhari(tone ya mrisho kwenye salam kwa mjomb rudi)

nasubiri JAWABU..au niwachagulie mji mnipe jibu..Nang'urukuru

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mbona hawaulizii nywele?? bado wadogo nini?? kama ndevu, mav%@& na bustani yamapenzi (love garden / garden love?)
kuna jamaa alijikata kichwani ili kuona kama kuna mizizi yanywere, hakuiona, alilia na kusaga meno

PASSION4FASHION.TZ said...

Mmmh!kumbe kina vilaza tuko wengi,hapa kuna mengi ya kujifunza.

Anonymous said...

mimi najua ila sitaki kuwaambia, mkitaka niombeni niwaambie

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina 10.02 pm, tafadhali nakuomba uniambia napiga hata magoti TAFADHALI.

Anonymous said...

Nshaghairi mie, sisemi!! mkitaka tafuteni mtandaoni nimeweka majibu!!

Mija Shija Sayi said...

Anony tafadhali tuko chini ya miguu yako.....

Kareni Michael said...

Kwa kweli hatamimi nimeona swali ni ngumu kidogo mimi kwa jibu langu ni hivi binadamu wanapozeeka meno yao hupekechwa na wadudu na baadaye kung'ooka