Hiii hadithi inanikumbusha mambo mengi sana sijui wenzangu mnasemaje?
Kulikuwa na baba mmoja aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. Siku moja yule wa mwisho akamwambia baba yake : baba mimi sasa ni mkubwa naomba haki yangu nataka kuondoka kwenda mbali kutafuta maisha. Baba yake akampa pesa nyingi tu. Akaondoka akaenda zake na pesa zote.
Muda si mrefu akapata marafiki wengi tu. akawa anakula na kunywa nao pamoja na yeye ndiye aliyekuwa analipa kila kitu.
Lakini muda si mrefu pesa zote zikamwishia. Akawa hana kitu cha kula. Marafiki zake wote hawakumpa wala kumsaidia chochote isipokuwa walimtupa barabarani.
Siku moja akaondoka akaenda kwa mkulima mmoja na kusema ya kwamba anaomba chakula, aina yoyote ile, na halafu atafanya kazi kwake. Mkulima akamhurumia akampa chakula na akamwambia kazi yake ni kuchunga nguruwe wake.
Hata hiyo kijana bado alikuwa ana njaa. Akaanza kuwaza: kwa nini napata taabu hapa wakati baba yangu ana chakula kingi tu. Narudi nyumbani kwa baba tena. Nataka kufanya kazi kwa baba kuliko hapa.
Mara akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Na kusema baba, naomba radhi nimekosa. Ilibidi nisirudi na wala usinipokee tena hapa nyumbani kwako. Lakini baba kwa uchungu wa furaha akamkumbatia na kumpokea. Kwa furaha kubwa baba akamfanyia kijana wake sherehe kubwa kwa kufurahia kwa sababu kijana wake alikuwa amerudi tena kwake.
Kaka mtu akawa anarudi toka kazini(shambani) akakutana na babake asemaye. Mdogo wako amerudi tena nyumbani njoo tumsherehekee. Alipotea sasa amerudi tena.
Swali: Je? Hadithihii wewe inakufundisha nini?
Na je? ungekuwa wewe ni yule kaka mkubwa ungefanyaje?
Hebu sikiliza hapa lugha ya mwenzetu wasukuma mimi nimeipenda kwani nimeelewa neno moja moja hata hivyo najivunia lugha zetu za asili zinasikika.
Au kama hujaelewa hapo basi sikiliza hapa lugha yetu ya kiswahili
7 comments:
1. Tu wadhaifu.
2. Ningempa nami jembe kwa njia ya kumkaribisha.
Mimi nimejifunza kuwa tusiwe tunapotea
mwana mpotevu?? Sikili mimi masikini uvivu wangu Nyumbani, ukiwa huu njiani nakufa hapa kwa nini......................................................................
ila story according to the bible hujaimalizia, mwanampotevu ni yule aliyekuwa Nyumbani kwani baada ya kuwa ameambiwa kuwa yule karudi, alichukia sana, kwa hiyo yeye ndo alikuwa kapote vibaya kuliko wewe ulivyopotelea Sweeden
KAMALA YASINTA KAPOTELEA SWEDEN AU ANAISHI SWEDEN? REKEBISHA SENTENSI YAKO WEWE.....!!!!!!
1. kuna vitu vinatuzunguka na hatuvioni kuwa ni vya maana mpaka tuvikose ama tunyang'anywe ndo tunaanza kulalama
2. upotevu uko katika fikra tu. Yawezekana hata tuwadhaniao kuwa wamipotea bado wapo tu nasi japo hatuwaoni machoni.
Si yawezekana hata wewe ni mpotevu ktk maisha yako ama kazi yako? :-(
Nakubaliana na Komandoo KAMALA stori hii inamapungufu kutokana na niikumbukavyo, na kwa mapungufu yake inaathiri aina ya ujumbe utolewao nayo.:-(
Lakini kwangu naamini .....
Kupotea ni UBINADAMU na ni bonge la shule LABDA hata KULIKO kujichunga kwa kutokuanza ili usipotee!
Na pia fundisho la STORI hii ni kwamba ni MUHIMU mtu apotee ili wengi wapate nafasi ya kujifunza KUTOKANA NA HILO kama ionekanavyo hapa katika stori hii.
PIA,...
...stori hii inaweza kufanya mtu aogope kuwa mjasiliamali kwa ilivyokaakaa tu ki-tishatoto.:-(
story hi inafunza anayepotea akarudi kwao atapokelewa kama alivo fanya baba
waswahili wanasema mwenda tezi na omo marejeo ngamani ukienda baharini kuvua basi mwisho lazima urudi nchi kavu au unasemaje dadangu Yasint
pili inafunza anaye kosa tunatakiwa tumsamehe ndipo mungu atapotusamehe na sisi
Post a Comment