Thursday, February 4, 2010

SAYANSI YAKIRI BINADAMU HAFI, HUBADILIKA.

Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho.
Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mambo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona.

Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine.

Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu.
Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulimwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.

Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.
Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.

Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.

Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.

Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.

Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.

Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.

Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.

Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .

Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.

Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.

Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.

Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.

Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.

Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.

Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa.
Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili.

Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo.

Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika.
Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi.

Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo.

Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.

Habari hii nimeipata katika gazeti la Jitambue la huko nyumbani Tanzania, ambalo siku hizi halichapishwi tena baada mmiliki wake Munga Tehenan kufariki dunia.

12 comments:

Ramson said...

hii habari imenikumbusha kisa cha mtoto wa dada yangu ambaye alikuwa anatokewa na kitu kama Deja Vu! hivi, kila akienda mahali kwa mara ya kwanza alikuwa anadai kufika mahali hapo kabla, na alikuwa akisema vitu ambavyo vilikuwa vinawaacha watu na mshangao kutokana na kuacha maswali.
Wakati huo nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1984 na alikuwa ana miaka minne tu.
Alikuwa akitaka kupelekwa mahali ambapo hata siku moja hakuna aliyewahi kufikiria kwenda huko, kwa mfano Sumbawanga.....alitusuumbua sana.
hata hivyo alikuja kufariki miaka mitatu baadae na kabla ya kufa alikuwa akiwataja watu tusiowafahamu kuwa wanakuja kumchukua.

Miaka 20 baadae nilikutana na Hayati Munga Tehenan mtaalamu wa elimu ya utambuzi, na baada ya kumweleza kisa hicho cha mjomba wangu alinipa elimu ambayo ilinifanya niujue ukweli mpana zaidi juu ya sisi wanaadamu.

yawezekana hata wewe unayesoma hapa una roho ya mtu mwingine ndani yako.
Hivi umeshawahi kujiuliza kwamba kwa nini baadhi ya wazazi hulalamikia tabia za baadhi ya watoto wao kwa kusema kuwa hajui kama tabia ile ameipata wapi, kwani tabia hiyo haipo kwao, kwa mfano uasherati, ulevi, umbeya na tabia chafu zinazofanana na hizo?

kuna uwezekanao watoto hao ni miili katika roho za watu wengine ambao walikuwa na tabia chafu kabla ya vifo vyao.

Unakuta wakati mwingine wazazi wanasema "unavyomuona huyu mwanangu yaani ni baba yangu mdogo mtupu"
haiyumkini huyo ni baba yake mdogo ndani ya mwili wa mwanae.

Ahsante dada Yasinta kwa kutukumbusha makala za Jitambue, sikujua kuwa haya magazeti yalikuwa yanafika huko Sweden

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Ramson: Sawa lakini inawezekana ukazaliwa nyani ama mbwa? Yawezekana wale watu tunaowaona wakiwa na roho mbaya wakawa 'walipaswa' kuzaliwa kama mbwa lakini nguvu za maumbile zikawafanya watu? :-(

Kaluse na Kamala wanaweza kutweleza hapa hii maneno. Mie ningependa nizaliwe NYAU lakini naogopa kufukuzwa na MBWa...lol

NA wana-Utambuzi watuambie: kwa kisa kama cha huyo mtoto wa dadako suluhisho ni nini ili kuzuia asikufe?

Unknown said...

Kaka Chacha Wambura hili swala bado linafanyiwa utafiti na wanasayansi, na kama tulvyoona kuwa Mwansayansi Vikram Chauhan ameonesha njia na hivyo kuharakisha mchakato wa ugunduzi wa nadharia hiyo kuthibitishwa na wansayansi wengine.

Ni swala ambalo linawezekana lakini bado kuna kusigishana mno miongoni mwa wanasayansi wengine.

Kama ulivyosema kuwa wapo ambao huzaliwa mbwa au paka, haiyumkini ni kweli lakini hili linahitaji ushahidi wa kisayansi zaidi.
Tusubiri matokeo ya utafiti huo, na si muda mrefu tunaweza kupatiwa majibu.

chib said...

Makala hii imenivutia sana. Bado naitafakari sana tu.

Ila mimi nafikiri sikuwahi kuishi siku za nyuma, mbona sina kumbukumbu au maono ya kale!!
Kila nisikichokijua kinakuwa kigeni kweli kweli

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

jambo hili linaitwa re-incarnation
sio jambo geni na wala sio la kisayansi wala nini, ni ukweli mtupu.

sisi tulikuwepo, tupo na tutakuwepo. hisia za kujiaona kama uliwahiishi pahala fulani hutokea sana tukiwa wadogo, CHIB. rejea fikra za utotoni, za kufikiri uliwahi zaliwa pahala

pale FAJI kuna jamaa mmoja baada ya kufundishwa meditation a.k.a tahajudi, alienda na kuona wazazi wake wakifanya ngono iliyomleta yeye duniani!!! kama ahaitoshi, aliona jinsi zamani alivyokuwa mbwa kule Norway na kufa akazaliwa tanga

sisi ni uwepo na sio miili, miili ina mwisho sisi hatuna mwisho kwa hiyo tupo, tulikuwepo na tutakuwepo!

washangae mafisadi wanaotukuza miili yao, wewe! utalipa tu
hata Oprah aliwahi fanyia utaifiti jambo hili

jifunze meditation na ukitaka utaona maisha yako ya zamani

hata Yesu ni reinacanation ya watu fulani fulani kama inavyojionyesha

so ni mambo amabayo yapo na sio imani,ni kwa meditation

chib said...

@Kamala: Hm!

Yasinta Ngonyani said...

Nimenukuu:- Ahsante dada Yasinta kwa kutukumbusha makala za Jitambue, sikujua kuwa haya magazeti yalikuwa yanafika huko Sweden" mwisho wa kunukuu, Kaka Ramson sikai huku tu huwa naenda nyumbani, na mwaka jana nilipokuwa nyumbani kwa vile babangu ni mpenzi wa magezeti hayo na ameyatunza, Kwa hhiyo mwaka jana nilipokuwa huku nikayasoma na kuchukua /nikapewa baadhi na kuja nayo huku.

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

PASSION4FASHION.TZ said...

Mmmh,ni mengi ambayo wengi hatuamini au hatuyajui lakini yapo na yataendelea kuwepo,binadamu hufa mwili lakini roho haifi ndio maana unaambiwa mtu anapokufa huwa na uwezo wakusikia kila kitu na isipokuwa uwezo wa kuongea tena haupo wa kufanya chochote huwezi ni kwa kuwa mwili wako umekufa lakini roho yako bado iko hai.

Anonymous said...

It was and with me.

Anonymous said...

Instead of criticising advise the problem decision.

Anonymous said...

It's probably a silly question, but when I miss a tv show and downloaded from BitTorrent/Mininova, it sounds like Dolby Digital, but it doesn't sound like it's in Stereo or 5/1. Is it? Or do I have to download someother program to download in Stereo or 5.1?
[url=http://www.topvideoconverter.com/asf-converter/]asf converter[/url]