Tuesday, February 9, 2010

Kibanga Ampiga Mkoloni



Nasoma kitabu cha Tujifunze Lugha Yetu
Wapendwa

Jana niliposti hapa kijiweni http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/02/kibanga-ampiga-mkoloni.html juu ya kisanga cha Kibanga kumbonda mkoloni. Awali nilitaka tu kuwakumbusha wanakijiwe juu ya stori hii lakini cha kushangaza Mt. Simon http://simon-kitururu.blogspot.com/na Chacha Ng’wanambiti! wamekuja na hoja nyingine ambazo haziwezi kupita bila kujadiliwa.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
kwa kung'ang'ania bakora mkoloni ana nguvu na jeuri!Je si kuna wakati tunag'ang'ania mambo hata yasofaa huku tukijiona tuna maguvu na jeuri ya kufanya tutakavo hata kama tunaumiza wengine? :-(
February 9, 2010 12:04 AM

SIMON KITURURU said...
Nimeipenda sana staili ya ngwala a.k.a kubwengana ya Mheshimiwa mpole Kibanga.Lakini bado :``Siku hizi kijiji cha Kwachaga kina maendele mazuri ya kilimo na mifugo. Maendeleo yote yamepatikana kwa sababu ya uongozi bora wa Serikali ya wananchi.´´- inanitamanisha nitamani kwenda huko KWACHANGA kwa kuwa BADO najiuliza zaidi kuwa;- hivi huko KWACHANGA ni Tanzania? Kwa maana nahisi viongozi wao wangeifaa kweli SERIKALI ya Tanzania baada ya Watanzania kumuondoa TANZANIA Mkoloni.:-(Ngojea niwashangilie washindi,Kibanga OYEEE! Ukoloni mamboleo OYEE!Nawaza tu!:-(
February 9, 2010 12:55 AM

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
na kwa mtindo wa ushangiliaji wa mt. simon akiwa na glass ya komoni a.k.a ze bia mkoni, nina wasiwasi kama viongozi wetu watazinduka na kuuona ukweli wa kuwa twaweza kujiletea maendeleo wenyewe bila wakoloni:-(katika dunia ya sasa Kibanga angeweza kuonekana kichaa! je unadhani twahitaji vichaa wengi wa kuwazindua viongozi wetu kama alivozinduliwa waziri mkuu wa Italia?Samahani jamani, labda naanza kurukwa na akili :-( Lakini kama ndivo msinambie miye ndo niende kuwazindua hao walolala :-(
February 9, 2010 6:52 AM

SIMON KITURURU said...
@Kadinali Chacha Ng'wanambiti: Unauhakika Kibanga alivyompiga Mkoloni ni kweli Mkoloni aliondoka na Ukoloni wake?Si wajua kuwa jambo kubwa litofautishalo ukoloni na kwenda haja msalani a.k.a CHOONI ni kwamba UKOLONI hauhitaji Mkoloni awepo katika KOLONI kama Haja ihitajivyo ajisaidiaye chooni awe CHOONI?
February 9, 2010 10:49 AM

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
@Mt. Simon: ni kweli kabisa mkoloni hakuondoka na ukoloni wake kwa kuwa kuna bado vijeba ambavyo ukiviangalia saaaaaana utastukia kuwa ni vikolini katika nguo za rangi ya kijani/njano :-(na kuhusu choo nadhani silazima mtu aende chooni kwani katika baadhi ya makabila kama la kwangu wawezakuta msitu wa jirani umesheheni uyoga kwa kuwa kuna mbolea-kinyesi cha mtu :-( na waweza ukakuta karibu na palipo na mzigo wa kinyesi aidha kuna kuna aidha jiwe ama nyasi badala ya ukoloni wa toilet paper :-(lakini, ni wangapi kati yetu tumefikiria kuhusu ujenzi wa choo au kujisitiri vichakani katika staili ya kumfukuza mkoloni mawazoni?Una hakika wewe si mkoloni ndani ya Utakatifu? :-(


Je WADAU, ni mafunzo gani tunayoweza kutohoa katika hadithi hii? Je ni kweli viongozi wa kijiji cha kibanga wanaweza kuwa suluhisho la ombwe la uongozi katika Tanzania yetu ya leo?

14 comments:

Simon Kitururu said...

@Yasinta:
Labda hawawezi.


Mkoloni mwenyewe kwa kunukuu stori inaonyesha alikuwa mmoja PEKE YAKE hapo kijijini KWAO.


Na kutokana na alivyobadili tabia GHAFLA kwa kunyang'anywa tu bakora INAONYESHA hata gobole hakuwa nalo.:-(

AU?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Mt. Simon: yawezekana pia wakaweza. Si unakumbuka tulikuwa na Nyerere mmoja ambaye alishirikiana na wazee wengine kuleta 'UHURU'?

Nazinguka na dhana kuwa ukiwa na silaha fulani na ukanyang'anywa unabadili tabia :-( Unadhani kuwa kama angekuwa gobole angeweza kuwamaliza hao ama wakati ulifika na akaona kuwa hata akienda na gobole aweza kukumbana na kijeba KIBANGA na kikamcharaza pia na gobole lake?

na je si yawezekana bakora ya mzungu ikawa ni gobole kwa baadhi ya mazingira? Ama umisahau stori ya Goliati na Daudi?

Je ni kitu gani kinatufanya tuone kuwa hayo ambayo aliyafanya kijeba KIBANGA hatuwezi kuyafanya ili kutuliza mzuka wa Da Yasinta katika KUZIBA OMBWE la uongozi katika Tanzania yake a.k.a Danganyika ambayo muzungu akija na $1 kuwekeza anaondoka na mamilioni ya $?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nyerere alileta uhuru???? kutoka wapi? huo uhuru aliutoa wapi?

Nyerere ndo kibanga? ila cha kukumbuka zaidi ni kwamba hata gobole hakuwa nayo kwani aliacha tabia ya kutupeleka kwa nguvu akaja kwa njia yakutongoza

Mija Shija Sayi said...

Mkoloni alipopewa kichapo na kunyang'anywa bakora yake alishika adabu na kukubali kwamba kiburi si Maungwana.

Nashawishika pia hivi VIJISENTI vinavyowazingua wakoloni mamboleo wa TZ vikinyang'anywa mikononi mwao na serikali kuziba mianya yote ya kuvipata, nao watashika adabu na kila wakati kukumbuka kwamba Kiburi si maungwana.

@Yasinta je unaweza ukakipiga picha hicho kitabu natamani nione kava lake la juu lilikuwaje maana nimesahau.

Yasinta Ngonyani said...

Da mija komputa yangu ina virus picha nimepiga kuwa na subitra nitaweka.

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu "nyerere alileta uhuru???? kutoka wapi? huo uhuru aliutoa wapi?" mwisho wa kunukuu, Kamala sisi wengine tunaelewa ya kwamba Nyerere ndiye aliyeleta uhuru. Je wewe unafikiri ni nani alileta uhuru na je huamini kama tupo huru?

Mija Shija Sayi said...

@Kamala aliutoa UNO au unabisha?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Yasinta labda wewe uko huru, mimi sijui kama niko huru kama asemavyo kitururu, ukijisikia kujamba unabana, ukistaka kwenda chooni unajifungia nk nk, je uko huru?

damija uhuru uko UNO? mbona wafanyakazi wa UNO nao hawako huru saa nyingine? au Nyerer aliutoa wote na kuuleta Tz?

Yasinta Ngonyani said...

Da Mija nimeiweka ile picha au kava la kitabu. Upendo Daima

Mija Shija Sayi said...

Jamani sio siri kuna watu itakuwa ngumu kuzeeka na mmoja wao ni Da Yasinta. Asante kwa Picha ya kitabu.

@Kamala inategemea unaongelea Uhuru gani?

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu "Jamani sio siri kuna watu itakuwa ngumu kuzeeka na mmoja wao ni Da Yasinta." Da mija unamaanisha nini hapa?

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Da Mija: mimi no mmojawapo wa watu wasioshabikia kuishi maisha marefu wenyewe lakini wanashabikia wengine kuishi maisha marefu.

Hebu tujuze mwanakwetu, umitumia kigezo gani kusema ati Da Yasinta ataishi maisha marefu a.k.a KUTOZEEKA mapema?

Mija Shija Sayi said...

Leo hii ukiambiwa Yasinta ana miaka 18-24 unakubali, Mimi kabla sijamjua vizuri Yasinta nilikuwa nadhani yuko Sweden kimasomo. Siku nilipomuona Camilla nilishika tama kama Brown (Si mnakikumbuka kitabu cha BROWN ASHIKA TAMA?)

Maana yangu ni kwamba ana Udongo mzuri.

Yasinta Ngonyani said...

Oh kumbe! Da Mija Asante sana lakini inawezekana wewe na mimi mimi ni mkubwa:-) Asante kwa kujibu kwa haraka pia kwani nilikuwa natafakari na sikupata jibu.