Thursday, December 29, 2011

YOU CAN HIRE THIS CAR IN DAR ES SALAAM!!!


The car with a driver, will only cost you 500SEK + petrol for one day in the city of Dar-es-Salaam.
About 60 Euro, 48 pounds, or 75 USD.For trips outside Dar contact us.
Torbjörn Klaesson +46 70 2217044mail: matetereks@gmail.com OR....
Yasinta Ngonyani +46 70 2569176 mail: ruhuwiko@gmail.com


10 comments:

Mija Shija Sayi said...

Asante kwa ujumbe Mrs Klaesson..

Uchokozi: Mrs Klaesson kikwetu unatakiwa ubadili jina unapoolewa..

Baraka kwenu..

Goodman Manyanya Phiri said...

Uchokozi zaidi:

Hiro ni gari kweri au ngurue wa pori? Pua gani hiro?

On a more sober note: Asante kwa kutufahamisha, Da'Yasinta Klaesson! Unajua safari za Tanzania haswa kwa wakati wa mvua kama huu si mama lele.

Mtu unaweza kabisa ukajikuta umelala porini tena kwenye matope kabisa ukiwa unatumia magari haya madogo-madogo ya kusafiria mjini!

@Mija

Naipenda HAIRDO yako. Kama nayiona mara ya kwanza vile...au nilikuwa kipofu... safi sana. Heri kwenu wote kwa myaka mpya kesho au keshokutwa hivyohivyo!

sam mbogo said...

Ukiolewa kwa kina mija inabidi ubadili jina,hasa la ukoo. uchokozi-wewe da mija unaitwaje sasa.....Mrs..... patamu hapo.wangu kashindwa kulitumia jina langu mwisho, hivyo liko katikati,yaani,......mbogo.......
nawatakia wote kheri ya mwaka mpya. kaka s.

ray njau said...

Haya ndugu wananji piasara ni matagaso na matangaso ndo hayo mangi.Mama Klaesson tumeopokea ujumbe wako kwa kweli ila tu hapa naona namba za simu za China na gari ipo Dar es salaam na lugha iliyotumika ndiyo ile ya bi mkubwa wa Ukonga.Hapa naona maswali ni mengi majibu huenda yakawa ya kuchakachua.Waheshimiwa wadau naondoa senti kumi na tano na siungi hoja mkono kwa asilimia kadhaa.

chib said...

Kama kawaida sisi tumezoea punguzo, hakyanani hata ukisema senti tano kwa siku sisi tutaomba bei ya mwisho....

Yasinta Ngonyani said...

Nafurahi kama ujumbe umepokelewa
Mija wala mimi si mchokozi, kuolewa si kubadili jina na je nani kasema mimi nimeolewa(funga ndoa?)..LOL

Kaka Manyanya ni gari na ni zuri tu ukiwa unaliendesha hutapenda kuacha.

Kaka Sam! Ahsante kwa kuuliza swali hili ....
Kaka Ray: Nashukuru kwa kuupokea ujumbe...nanukuu "Mama Klaesson tumeopokea ujumbe wako kwa kweli ila tu hapa naona namba za simu za China na gari ipo Dar es salaam na lugha iliyotumika ndiyo ile ya bi mkubwa wa Ukonga." mwisho wa kunukuu..Hapa tatizo ni namba au tatizo nini hujawahi kuona mtu anaishi TZ na ana namba ya aina hiyo?

Kaka Chib! Ni maelewano tu!

Mija Shija Sayi said...

@Kaka Sam!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Yasinta umenitafakarisha hapa ila nitarudi ngoja nikajiweke vizuri kwa ubishi..

Anonymous said...

Kuna maoni yaliyotolewa juu ya namba za cm. Nafikiri hukumuelewa, tupe namba za tz pia. Ivi mie niko Africa nitaweza kweli piga cm uswid? Ni vema kuwa na namba karibu na gari lilipo.

ray njau said...

@Mama Klaesson;
Hakika nimekusoma na swali la nyongeza limeyeyuka.
Karibu Dar es salaam,Karibu Tanzania na usafiri tumeupokea na kilichobaki ni kwa wadau kuonyesha ushirikiano.Kizuri kula na ndugu zako na kichungu meza mwenyewe.

mwl. Klayson said...

Anonymous said...
Kama hunauwezo kupiga simu mbali, utaweza kulipia kodi ya gari?
Subiri, mwaka mwingine kufungua maofisi miji mingine.