Wednesday, December 28, 2011

JAMANI, MBOGA, MBOGA, MCHICHA UNAPITA MBOGA YA MCHANA/JIONI!!!

Jipatie mboga ya haraka kwa mchana huu au labda jioni ...bei pouwa .

14 comments:

Mija Shija Sayi said...

Afrika tuna raha sana, yaani kitu fresh...

Yasinta Ngonyani said...

Mija nimeipenda picha yako utadhani kahinza kadebedebe:-) Ni kweli tuna raha sana kuingia shambani kuchuma mboga na kupika majokofu ya nini hahahaha raha sana.

Mija Shija Sayi said...

Kahinza ndo nani tena Yasinta? Asante sana.

Yasinta Ngonyani said...

Kahinza ni kibena maana yake kasichana. Vipi umenunua huo mchicha...

sam mbogo said...

kwa lugha ya sauzi, msichana, wanaita NTOMBI,wasichana wanaitwa , AMANTOMBIZANA. nawatakia kheri ya mwaka mpya wadada nyie. ndimi mimi kaka yenu ,kaka s

Anonymous said...

MBOGA ZILIZOJAA VINYESI!! ANGALIENI SANA MSIONE VIMESTAWI HAPO, NI UCHAFU USIOWEZA KUAMINI, BORA KULIMA SHAMBANI KWAKO, NILIENDA KUNUNUA MCHICHA MANDELA RD, WANA SHAMBA KUBWA SANA LIMESTAWI MNO, YAANI KWA MACHO PANAPENDEZA MNO, LAKINI KAMA MUNGU NIKAAMUA KUINGIA KIDOGO NDANI YA SHAMBA NIANGALIE UTAALAMU MAANA NI SHAMBA ZURI MNO, HEE! NILICHOKISHUHUDIA SIKUAMINI, NILIPOINGIA NIKAENDA KWA KAKA AMBAYE AMESIMAMA KWENYE KIPANDE CHAKE MAANA KUNA WAKULIMA WENGI HAPO KILA MTU ANAKIPANDE CHAKE, BASI NIKAMWAMBIA KAKA NIMEPENDA MCHICHA WAKO UMESTAWI VIZURI NAOMBA WA ELFU MOJA, KAKA WA WATU KWA UAMINIFU NA UKWELI AKANIAMBIA KATOKA KUMWAGILIA HIVYO HAUUZI MPAKA UKAUKE!! NIKAMWAMBIA SI MAJI TU KAKA NICHUMIE, AKANIJIBU AAH DADA NA MAJI YETU HAYA, NIKAMUULIZA MAJI YAKOJE, AKAJIBU YA MTARO, NIKAMUULIZA MTARO UKWAPI AKANIONYESHA! JAMANI NI KINYESI KINAPITA MCHANA KWEUPE, MAJI SI MAJI NI VINYESI, NIKAMUULIZA KAKA KWELI MNAMWAGILIA MAJI YENYE KINYESI! AKANIJIBU DADA DAR MAJI SHIDA NDIO MAANA HATUUZI UKIWA UMELOA! NA HAPO WADAU KUNA KINA DADA KIBAO KAMAHUYO KWENYE PICHA WAMEKUJA KUNUNUA WAPELEKE MITAANI! KUWENI WAANGALIFU SANA, TOKA SIKU HIYO SIJANUNUA MBOGA MTAANI HATA AKISEMA OHH NIMETOA MKOANI.. NI UONGO MKUBWA. BE AWARE PEOPLE, LOVE YOUR SELF, NUNUA SHAMBA CHIMBA KISIMA WEKA KAKA ATAKAYEKUWA ANALIMA, KWANZA UTAPATA MBOGA SALAMA, PIA UMETOA AJIRA, MWISHO INAWEZA IKAWA BIASHARA UNAUZIA WAZALENDO MBOGA SAFI NA SALAMA.

Swahili na Waswahili said...

Ahsante kwakututamanisha da'Yasinta,baraka kwenu nyote!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Ngoja siku yake nifanya kitu ambacho sijawahi kufanya ..Umenifungua macho hapa.Ahsante:-)

Usiye na jina! nina swali moja je hicho kinyesi ni cha wanyama au binadamu?..Halafu kama ulivyosema ni kweli kabisa ni vizuri kulima mwenyewe kwani hata sio kazi mwenyewe hapa nina kasehemu huwa nalima. Kwanza ni kubana matumizi, na halafu ni vizuri kujishughulisha.
Rachel! nilijua utalalamika kuwa nakutamanisha:-)

Mija Shija Sayi said...

Yasinta nilitaka kununua huo mchicha lakini bahati mbaya nikapitia hapa tena ndo nikakutana na hiyo tahadhari ya Anonymous, basi nimeona nishike jembe mwenyewe kwani kama ulivyosema sio hata kazi...

Baraka kwenu wote hasa kaka s..

Swahili na Waswahili said...

Kwikwikwi ngoja nije hukohuko nijilie vitu fresh kwa dada yangu!!

Yasinta Ngonyani said...

Mija! andaa majembe matatu moja lako, moja langu na moja la Rachel nakwambia tutalima na kula na hata mwingine kuuza...Rachel nakwambia wakati wa joto njoo utaona mchicha wangu pia mboga maboga.

Mija Shija Sayi said...

Nimekupata Yasinta nitayaandaa, ila tuwe makini na Muke ya Mubena anaweza akatutoa Knock-out anaoneka analiweza sana jembe...

Baraka kwenu wote..

Yasinta Ngonyani said...

Usihofu muke wa mubena hawezi kunishinda mimi si unajua nimeishi kule ubenani:-)

Swahili na Waswahili said...

Yaani ninyi msifanye masihara na Muke ya Mubena!!!tehtehteh,ngoja nizichange dadake!