Sunday, December 25, 2011

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE NOELI NJEMA KWA WIMBO HUU...


Kristmas njema sana ndugu zanguni ...Mwenzeni nimepata ile hisia kuwa nipo kanisani Makwai/lundo au sijui Ruhuwiko na naimba nyimbo hizi....yaani basi tu ..JUMAPILI NA KRISTMAS NJEMA KWA WOTE.

8 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Krismasi njema kwako pia Da Yasinta. Hebu Mungu na Aendelee kukubariki wewe pamoja na familia yako na wapendwa wako wote. Na mwaka mpya ujao ukawe bora zaidi na wenye kuweka rekodi kwa kila jambo jema!

Malkiory Matiya said...

Heri na kwako pia Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Matondo! Ahsante sana. Pia Mungu aandelee kukubariki wewe na familia pia. Na nawatakieni kila jema na mwaka 2012 uwe wa amani na mafanikio.

Kaka Malkiory! Nashukuru kwa salamu ni jambo zuri kutakiana kheri kwa kipindi hiki.Uwe na amani na kheri sana kwa Kristmas pia mwaka mpya.

Baraka Chibiriti said...

ASANTE SANA DADA YASINTA....PIA KWAKO NA FAMILIA YAKO YOTE DADA YASINTA...HERI NYINGI SANA KATIKA SIKUKUU HII NZIRI YA KUZALIWA BWANA WETU YESU KRISTU.

NN Mhango said...

Da Yacinta,
Hata kama nimechelewa angalau nimefika kukutakieni heri ya Krismas na mwaka mpya wenye kila manono. Nimefurahi kukutana na wapendwa wangu Masangu Matondo, Malkiory Matiya wote ni MM utadhani wameambiana! Ningekuwa nakumbuka kingoni basi ningekutakia kila la heri kwa lugha hii adhimu. Kwa ufupi bila kuchonga sana, nakutakia kila la heri wewe na familia yako hapo Uropa na Ungonini.

Penina Simon said...

Ahsante Mungu awe nawe sku zote pamoja na familia yako hadi mwaka uishe salama.

Mija Shija Sayi said...

Baraka kwako dada.

Yasinta Ngonyani said...

Naamini wote mmeshereheke vizuri Christmas..Binafsi hakuwa nzuri sana nilikuwa na homa ila nashukuru Mungu naendelea vizuri. Ahsantena sana wote kwa kutochoka kupita hgapa na kuacha kitu. Mwenyezi Mungu na awabariki. Kwani bila uwepo wenu na ushirikiano wenu nisingekuwa hapa nilipo/kublog. PAMOJA DAIMA.