Thursday, December 8, 2011

KUJIFUNZA/KUJITEGEMEA MAISHA/KAZI ZA NYUMBANI!! AU MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO!!

Tulipokuwa nyumbani mwezi wa sita mwishoni mpaka wa nane mwanzoni bahati nzuri ulikuwa ni msimu wa kuvuna. Tulimkuta Mzee ngonyani/babu amevuna mahindi. Na hapa mnamwona kijana Erik akimsaidia babu kupiga mahindi, kwa babu Songea Ruhuwiko.



Baada ya kazi nzito ya kupiga mahindi nguo zilikuwa zimechafuka kwa hiyo ni lazima kufua na hapa mnamwona anafua nguo zake....hapa ni Songea Ruhuwiko ....


Dada mtu naye siku yake ya dobi ikaja kama mnavyoona naye anafua nguo zake. Hii /hizi kazi ni moja ya kujifunza kuishi kwa kujitegemea.Uzuri wake maji tulikuwa nayo humu humu uani.

MAISHA NI KUJIFUNZA.

11 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

hongera sana kwa malezi mazuri unayowapa watoto ..kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...


tutafika tu

Anonymous said...

hongera sana dada yasinta kwa malezi yako mazuri maana kuna watu wengine wakishakuwa ulaya basi ni mambo ya uzungu tu mambo ya kumfundisha mtoto jinsi ya kujitegemea inakuwantabu tupu waswahili husema mzarau kwao ni mtumwa kweli dada ninavyokuonaga wewe pamoja na kukaa kwako nje ya nchi lakini hujasahau mila na desturi za nyumbani tz hiyo ni safi sana maana kuna wengi wakikaa nje kidogo tu full majivuno na uzungu mwiiingi hata watoto wao hawataki wazungumze kiswahili huo ni ulimbukeni wa kutupwa big up dada yasinta nakupenda sana maana uanaonekana una utu na busara sana uabarikiwe sana na familia yako

Baraka Chibiriti said...

Safi sanaaa...nimependa sana hii, na hongera sana Dada Yasinta kwa kuwa na vijana wachapa kazi.

Rachel Siwa said...

Hongera sana da'Yasinta yaani nakukubali mnoooooo duuhh wewe ni mama haswa na Mungu azidi kuwabariki wewe na familia yako, pia wote wataopita hapa.Mimi penda sana wewe!

Goodman Manyanya Phiri said...

"Mama lea mtoto!"

Mija Shija Sayi said...

MmmH Watoto wa shoka! Hapa halaumiwi mzazi.

Hongera Yasinta.

Mija Shija Sayi said...

samahani nilisahau kitu,

Hawa watoto kama wanaweza kazi hivi, basi nina hakika kabisa hutapata shida mdogo wao akija.

Abarikiwe atakayepitia hapa.

Yasinta Ngonyani said...

Edo! wengi wanasema kulea mimba si kazi ila kulea ndo kazi ni kweli naamini. Na ahsante kwa kuona kuwa nawafunza wajombao maisha haya niliyopitia mimi.Ni kweli tutafika tu.
Usiye na jina mimi siona sababu ya kusahau kwangu au kujifanya kuwa nimesahau. Ahsante sana kwa kulisema hilo ni kweli wapo tena wengi tu.
Kaka Baraka! Nafurahi kama umependa hii na Ahsante kwa kunipa hongera ni kwamba najitahidi ili wajue tamadani zote huwezi kujua...

Rachel! Najitahidi kuwaonyesha tamaduni zangu ili wasipate shida waendapo . Nawe unapendwa pia na wewe kwa vile umepita hapa basi tayari umebarikiwa.
Kaka mkubwa Phiri! najitahidi kuwalea kadiri nilivyolelewa mimi mwenyewe pia.

Mija! ni kweli mtoto wa shoka ni shoka au mtoto wa nyoka ni nyoka. Ahsante ndugu wangu...hahahaaaaa
haaaaaa mwe nimecheka kwelikweli mbaka mbavu hazina hali ETI UNA UHAKIKA KABISA MDOGO WAO AKIJA HATAPATA SHIDA HA HA HAAAA. nawe pia kwa vile umepita hapa basi nawe umebarikiwa . HAYA MBARIKIWE WOTE MLIOPITA HAPA NA wataopita hapa na pia amani na upendo viwe nanyi.

Penina Simon said...

Hongera, nimeipenda hii, watoto lazima wazoee kazi, vinginevyo watapata shida wakiwa wakubwa
hata kuosha sahani itakuwa kazi.

Anonymous said...

Umekuwa mzalendo wa maisha ya ulikotoka.Hiyo safi mnoooooooooo!! wengi wanawafunza ya huko walikolowea tu na kudharau walikotoka.Pongezi sana.Mimi nina watoto wangu hapa USA,huwa siwaruhusu kufua nguo zao kwenye mashine, nawachagulia ni nguo gani waoshe kwa mashine na nguo gani waoshe kwa mikono kama wanavyofanya wanao hapo.

Yasinta Ngonyani said...

Dada P. Ahsante sana Si unajua tupo safarini sisi binadamu.

Usiye na jina! Hongera na wewe kwani hawa watoto hawataishi na sisi milele watahitaji kuishi peke yao. Kwa hiyo inabidi kuwafunza kama sisi tulivyofunzwa. Hata kupika vyakula inabidi kuwafundisha. Mbarikiwe sana wote mnaopita hapa.