Friday, September 2, 2011

CHAKULA NILICHOANDAA na KULA JIONI LEO/IJUMAA HII KARIBUNI TUJUMUIKE!!

Kwenye sahani hii ni :- Wali (mchele wa kutoka nyumbani tena kule kunakosemekana ni mchele bora kuliko yote hasa Tanzania sio kwingine tena ni KYELA).... mshikaki wa kuku na kachumbali ..kitelemshio ni maji lakini usiogope kuna vinyaji vingine kwa anayependelea. KARIBUNI TUJUMUIKE ..JIONI NJEMA...

12 comments:

chib said...

Hapa tunatafutana visa tu :-)

Christian Sikapundwa said...

TUNA SHUKURU KUJUMUIKA KATIKA MLO HUO ULIYO ANDAA,

Anonymous said...

Naona hakuna pilipili katika kachumbali,vipi ni wali nazi ama?Napenda sana mlo huo ulioandaa, asante, ubarikiwe

Anonymous said...

ASANTE DADA YASTANTA LAKINI MIMI NAONA INGEKUWA BORA KAMA NI UGALI MAANA KAMA NI WALI UTAKULA NA KIJIKO AU MKONO RAHA YA UGALI NA MSHIKAKI ULE NA MKONO AU VIPI BWANAE

Anonymous said...

ASANTE DADA YASTANTA LAKINI MIMI NAONA INGEKUWA BORA KAMA NI UGALI MAANA KAMA NI WALI UTAKULA NA KIJIKO AU MKONO RAHA YA UGALI NA MSHIKAKI ULE NA MKONO AU VIPI BWANAE

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Chib! kwanini iwe visa?

Christian! kwanza nasema karibu tena maana ulipotea kidogo. Karibu sana.

Usiye na jina wa 2/9 10:40 PM ! usiwe na wasiwasi pilipili ipo tena pilipili mbuzi.

usiye na jina wa 12:39 AM! Wala usipate taabu ugali utakuwepo kwa ajili yako...Ni kweli ugali ni bora kwa mshikaki:-)

Kamala! mbona mh? vipi?

ray njau said...

KUENDAKO HISANI HAKURUDI NUKSANI BALI SHUKRANI.UKARIMU WAKO WA KINGONI
UNATHAMINIWA SANA.ASANTE SANA!

Simon Kitururu said...

Mmmmh! Wali na KACHUMBARI mpaka MSHIKAKI havitoshi kwetu kijiweni ! Huo si matonge mawili rijali akifinyanga mlo?:-(

Asante lakini!
Ila funga jiko kwa kuwa tunaweza kwenda huko ukilala.... kwa kuwa lazima ukoko na makombo yapo huko!:-(

Yasinta Ngonyani said...

hahahaha! Simon huo wali ni mwingi sana... halafu umenifanya mpaka nicheke kidogo eti nifunge mlango...Haya Mtakatifu!!!!

John Mwaipopo said...

mie hivyo vinywaji vingine tu, ndio nataka!

Yasinta Ngonyani said...

Ha ha hahaaa! watu weweeee, kaka John wala usipate tanu kuna kila kinywaji hadi ULANZI:-)