Thursday, September 8, 2011

MATITI NI CHAKULA CHA MTOTO AU?

Sijui kwa ajili ya kukosa watoto au Kweli huu ni UUNGWANA kweli kumnyonyesha mbuzi?



Na huyo naye anamnyonyesha mtoto wa ndama kisa? Sijui akimngáta hapo atasema nini?
Hapa sawa, mama akimpa mtoto chakula ambacho ndicho chakula bora sana kwa watoto wachanga. Ila kuna simulizi nimeisikia kuwa, wanaume wengi huwa wanaona WIVU sana wakati mama/mke wake amnyonyeshapo mtoto. Hasa mtoto wa kiume. Sijui wenzangu nanyi mmewahi kusikia? Na kama kweli kwanini sio anyonyeshwapo mtoto wa kike?

13 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"Wanaume wengi huwa wanaona WIVU sana wakati mama/mke wake amnyonyeshapo mtoto. Hasa mtoto wa kiume. Sijui wenzangu nanyi mmewahi kusikia? Na kama kweli kwa nini sio anyonyeshwapo mtoto wa kike?"

Kama sikosei suala hili lilishawahi kudokezwa na Mwanasaikolojia Sigmund Freud ambaye aliamini kuwa mvuto na misukumo ya kingono ndiyo hasa hutawala maisha ya binadamu. Mtoto wa kike humwonea wivu mamake kwani anataka kuwa karibu zaidi na babake (kingono) na mtoto wa kiume humwonea wivu babake kwani anataka kuwa karibu zaidi na mamake (kingono). Matamanio haya hata hivyo hufifia kwa kadri mtoto anavyokua na hatimaye kutoweka kabisa. Yanaposhindwa kutoweka basi ndiyo utakuta mambo ya "incest" yakiendelea.

Nadharia hii kwa wanaume hujulikana kama Oedipus complex (http://en.wikipedia.org/wiki/Oedipus_complex)

Mawazo haya ya Freud japo yalileta mtafaruku mkubwa, bado yanatumiwa na wanasaikolojia wengi wanapotafuta tiba za tabia kama "incest", matatizo ya ndoa, ngono na mengineyo.

Unaweza kumsoma Sigmund Freud hapa: http://en.wikipedia.org/wiki/Sigmund_Freud

sam mbogo said...

Bwana,Masangu.Haya mambo ya hawajamaa wana saikolojia,yanamambo sana,na mengine ndo hivyo kama asemavyo huyo mkali bwana sigmund Freud,nitampitia zaidi.kwa uzoefu wangu,mimi nina watoto wawili wakiume(madume ya mbegu) sijawahi kuwaza au kufikiri,pindipo mkewangu anapo myonyesha mtoto,kwamba mtoto anafaidi nyonyo ya mama,namimi nitake hapana.sijuwi labda watuambie,akina Da Yasinta,mtoto wa kiume anapo kunyonya wewe unajisikiaje?kaka S

Rachel Siwa said...

kwikwikwikwi kakas na wewe, haya nami ngoja nisikie mtyoto wa kiume akinyonya mama anajisikiaje,Dunia inamambo au watu wake ndiyowanamambo sijui.@Kaka Matondo ahsante kwa shule.

Goodman Manyanya Phiri said...

Jamaani wote mliechangia hadi sasa (kwa heshima lakini), MBUZI amepotelea wapi?

Au mumekwishamchinja nakummeza kwa kumwonea wivu kwa kunyonya lile ziwa?


Nimesoma pahala kunyonyesha kunapunguza unene sana kwa mwanamke. Kwa hiyo tusiwe na wivu wakuzidi: MBUZI ANAMSAIDIA MAMA KUKAA KAMA DOGODOGO VILE! (na kama mnawivu bado, fanyeni apointimente na huyo mama mzalendo, sidhani atakuwa mchoyo)


La mwisho kwako, Kapulya, mbona sisi binadamu wengi duniani (MAJORITY) tunakunywa maziwa kutoka ziwa la mbuzi wala sio hata ng'ombe ambao ni kiasi kidogo ukilinganisha na mbuzi lakini mbuzi hawajatufanyia maandamano ya wivu?

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Bwana Mbogo: Huyu Sigmund Freud asikutishe. Niliona tu nitoe dokezo hilo kwani pengine lingesaidia kutoa japo fununu tu kuhusu swali la Da Yasinta.

Ukweli hata hivyo ni kwamba nadharia hizi zinabakia kuwa nadharia tu na si vinginevyo. Tena tukumbuke kwamba nyingi zimetungwa katika mazingira ya Ulaya na sidhani kama zinazingatia sana tofauti za kitamaduni na kimazingira japo watungaji wake wanadai kwamba ni nadharia za kimalimwengu na zenye uwezo wa kuelezea tabia za binadamu wote. Kwa hivyo sitashangaa kama nadharia hizi zitakwama kule Afrika.

Hata wanasaikolojia wenyewe hawakubaliani kama kweli Freud alikuwa sahihi ama la kwani nadharia zake nyingi ni tata mno na hazithibitishiki kwa urahisi.

Japo hujawahi kuyaonea wivu hayo madume yako ya mbegu wakati yakifaidi matiti ya mkeo, pengine umefanya hivyo kihulkahulka tu na bila kujielewa (subconsciously).

Na kama Oedipus Complex iko sahihi basi si ajabu hayo madume yako ya mbegu yalikuwa yanatamani yakuue ili yamchukue mkeo moja kwa moja!

emu-three said...

Kwli duniani kuna mambo!

Simon Kitururu said...

Duh!

Anonymous said...

Kwa hiyo sakata lazima kuchangia .kumbe inawezekana? kama ndo hivyo basi hata sisi twaweza kunyonya kwa Ngombe and mbuzi? Du!! ama kweli Dunia Hadaa Ulimwengu shujaa?

John Fisher said...

Haya ni maajabu kwa binadamu wa kike kunyonyesha mnyama.
Hayo ya wanaume kuwa na wivu wakati amnyonyeshapo mtoto hayo ni mawazo ya mwana sikolojia Sigmund lakini nimewahi kusoma utafiti ambao umefanywa juhusu swala hili na wanasokolojia wa majuzi na kupika swala hili. Mwenyewe ni mwanaume na sijapata kuona wivu kamwe.....sijui wenzangu.
John Fisher Kanene

Anonymous said...

Wadosi wanajulikana duniani koote kwa imani za kijinga walizonazo, yani imani zao hata haziingi akili kichaa au mwehu ulimwambia afanye hivyo hafanyi, hawa watu namna yao peke yao imani hawana kabisa utakacho waambia wataabudu.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Ayiii....nadhani ni chakula CHA WOTE!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Bwana John Fisher Kanene;

Unaweza kutoa links au marejeo ya huo utafiti mpya kuhusu mawazo haya ya Freud? Ningependa kuusoma...

Asante

cytotec said...

obat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat telat bulan