Wednesday, September 28, 2011

MASUALA YA UBAKAJI NA KUPIGA WANAWAKE LINAZIDI KUWA KUBWA

Kama kawaida kile kipengele chetu cha marudio ya Makala/mada, picha au kwa ujumla tusemematukio mbalimbali kitujiacho siku ya kila siku ya JUMATANO ungana nami kujadili jambo hili.Ukitaka kusoma maoni yaliyotolewa na wasomaji mara ya kwanza bonyeza hapa.
Kweli huu ni ubinadamu jamani?
Dunia imeharibika watu wanazidi kupotoka, angalieni haya mambo yanavyozidi kuenea. Mambo kama vile unyanyasaji, kuna ukatili mwingi sana hapa duniani ambao zaidi ni juu ya wanawake na watoto. Hao ndio wanaopata shida zaidi. Ukatili ni kinyume na haki za binadamu na uko ukatili wa aina mbalimbali. Kuna vipigo, matusi, kulazimishwa kufanya mapenzi, kuna baadhi ya mila potofu kama vila ndoa za lazima, kuolewa ukiwa na umri mdogo, kurithi wajane nk.
Bado sijaelewa ni kitu gani kinawafanya wanaume wengine wawapige wanawake. Kwanini umpegi mwenzi wako? Je usipompiga uanaume wako utapotea? Na kuna raha gani kumpiga mwenzako kama mnyama? Na hata mnyama hairuhusiwi kumpiga. Hili suala la kubaka utasikia raha gani wakati mwenzako anapata maumivu yasiyo kifani. Na pia hajapenda.
Je? Mnafikiri hii inaweza kutokana na wengi wanaume wanafikiri wao ndio waamuzi wa kila kitu ndani ya nyumba? Na kwa nini watu wawili waliooana wasikaa chini na kujadiliana na kuona kosa liko wapi. Je? Ingekuwa kinyume ingakuwa sawa?

Au labda wengi wanafuata maandishi haya:- Mwanzo 3:16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako, kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumea, naye atakutawala.
Ndugu wasomaji/wanablog naomba mnisaidie kunipa jibu.

5 comments:

ray njau said...

Waefeso 5:1-33

1 Kwa hiyo, iweni waigaji wa Mungu, kama watoto wapendwa, 2 na endeleeni kutembea katika upendo, kama vile Kristo pia alivyowapenda ninyi na kujitoa mwenyewe kwa ajili yenu kuwa toleo na dhabihu kwa Mungu ili kuwa harufu tamu.

3 Uasherati na ukosefu wa usafi wa kila namna au pupa visitajwe hata kidogo katikati yenu, kama inavyowafaa watu watakatifu; 4 wala mwenendo wa aibu wala maneno ya kipumbavu wala mizaha michafu, mambo yasiyofaa, lakini badala ya hayo, utoaji wa shukrani. 5 Kwa maana mnajua hili, nanyi mnalitambua wenyewe, kwamba hakuna mwasherati au mtu asiye safi au mtu mwenye pupa—maana yake ni kuwa mwabudu-sanamu—aliye na urithi wowote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

6 Mtu yeyote asiwadanganye ninyi kwa maneno matupu, kwa maana kwa sababu ya mambo yaliyotangulia kusemwa ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wa kutotii. 7 Kwa hiyo msishirikiane pamoja nao; 8 kwa maana wakati mmoja ninyi mlikuwa giza, bali sasa ninyi ni nuru kuhusiana na Bwana. Endeleeni kutembea kama watoto wa nuru, 9 kwa maana matunda ya nuru yana kila namna ya wema na uadilifu na kweli. 10 Endeleeni kuhakikisha lile linalokubalika kwa Bwana; 11 na mwache kushirikiana pamoja nao katika matendo yasiyozaa matunda, ambayo ni ya giza, lakini badala yake muwe hata mkiyakaripia, 12 kwa maana mambo ambayo wao hutenda katika siri hata kuyasimulia ni aibu. 13 Basi mambo yote yanayokaripiwa yanafunuliwa na nuru, kwa maana kila jambo linalofunuliwa ni nuru. 14 Kwa hiyo yeye anasema: “Amka, Ee mwenye kulala usingizi, na ufufuke kutoka kwa wafu, na Kristo atakuangaza.”

15 Kwa hiyo endeleeni kuangalia sana kwamba jinsi mnavyotembea si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima, 16 mkijinunulia wakati unaofaa, kwa sababu siku hizi ni zenye uovu. 17 Kwa hiyo mwache kuwa wenye kukosa akili, bali endeleeni kufahamu yale yaliyo mapenzi ya Yehova. 18 Pia, msiwe mkilewa divai, ambayo ina upotovu ndani yake, bali endeleeni kujazwa na roho, 19 mkijisemesha kwa zaburi na sifa kwa Mungu na nyimbo za kiroho, mkiimba na kupiga muziki katika mioyo yenu kwa Yehova, 20 katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo mkimtolea shukrani sikuzote Mungu na Baba yetu kwa ajili ya mambo yote.

21 Jitiisheni kwa mmoja na mwenzake katika kumwogopa Kristo. 22 Wake na wajitiishe kwa waume zao kama kwa Bwana, 23 kwa sababu mume ni kichwa cha mke wake kama vile Kristo pia alivyo kichwa cha kutaniko, yeye akiwa mwokozi wa mwili huu. 24 Kwa kweli, kama kutaniko linavyojitiisha kwa Kristo, vivyo hivyo wanawake pia na wajitiishe kwa waume zao katika mambo yote. 25 Enyi waume, endeleeni kuwapenda wake zenu, kama vile Kristo pia alivyolipenda kutaniko na kujitoa mwenyewe kwa ajili yake, 26 ili alitakase, akilisafisha na kuliosha kwa maji kwa njia ya neno, 27 ili kujipa mwenyewe kutaniko likiwa na fahari, likiwa bila doa au kunyanzi au lolote la mambo hayo, bali ili liwe takatifu na bila dosari.

28 Vivyo hivyo waume wanapaswa kuwa wakiwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Yeye anayempenda mke wake anajipenda mwenyewe, 29 kwa maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake kwa vyovyote; bali huulisha na kuutunza kwa upendo, kama vile Kristo pia anavyolitendea kutaniko, 30 kwa sababu sisi ni viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 32 Siri hii takatifu ni kubwa. Sasa ninasema kwa habari ya Kristo na kutaniko. 33 Hata hivyo, pia, kila mtu mmoja-mmoja kati yenu na ampende hivyo mke wake kama vile anavyojipenda mwenyewe; kwa upande mwingine, mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.

ray njau said...

. Biblia husema kwamba mume ndiye kichwa cha familia yake. (1 Wakorintho 11:3) Ni lazima mume awe na mke mmoja tu. Wao wapaswa kuwa wameoana ifaavyo kisheria.—1 Timotheo 3:2; Tito 3:1.

2. Mume apaswa ampende mke wake kama vile ajipendavyo mwenyewe. Apaswa amtendee kwa njia ambayo Yesu huwatendea wafuasi wake. (Waefeso 5:25, 28, 29) Hapaswi kamwe kumpiga mke wake wala kumtenda vibaya kwa njia yoyote ile. Badala ya hivyo, apaswa amwonyeshe heshima na staha.—Wakolosai 3:19; 1 Petro 3:7.


Mungu huwatazamia wazazi wawafundishe watoto wao na kuwasahihisha
3. Baba apaswa afanye kazi kwa bidii ili kutunza familia yake. Ni lazima baba awaandalie mke na watoto wake chakula, mavazi, na nyumba. Ni lazima baba aandalie pia mahitaji ya kiroho ya familia yake. (1 Timotheo 5:8) Yeye huongoza katika kusaidia familia yake ijifunze kumhusu Mungu na makusudi Yake.—Kumbukumbu la Torati 6:4-9; Waefeso 6:4.

4. Mke apaswa awe msaidizi mwema kwa mume wake. (Mwanzo 2:18) Yeye apaswa kumsaidia mume wake katika kufundisha na kuzoeza watoto wao. (Mithali 1:8) Yehova humtaka mke ashughulikie familia yake kwa upendo. (Mithali 31:10, 15, 26, 27; Tito 2:4, 5) Yeye apaswa awe na staha yenye kina kwa mume wake.—Waefeso 5:22, 23, 33.

5. Mungu hutaka watoto wawatii wazazi wao. (Waefeso 6:1-3) Yeye huwatazamia wazazi wawafundishe na kuwasahihisha watoto wao. Wazazi huhitaji kutumia wakati pamoja na watoto wao na kujifunza Biblia pamoja nao, wakishughulikia mahitaji yao ya kiroho na ya kihisia-moyo. (Kumbukumbu la Torati 11:18, 19; Mithali 22:6, 15) Wazazi hawapaswi kamwe kuwatia nidhamu watoto wao kwa njia yenye ukali bila huruma au iliyo katili.—Wakolosai 3:21.


Baba mwenye upendo huiandalia familia yake kimwili na kiroho

6. Wenzi wa ndoa wanapokuwa na matatizo ya kupatana, wanapaswa kujaribu kutumia shauri la Biblia. Biblia hutuhimiza tuonyeshe upendo na kuwa wenye kusamehe. (Wakolosai 3:12-14) Neno la Mungu halipendekezi kutengana kuwa njia ya kusuluhisha matatizo madogo. Lakini huenda mke akachagua kumwacha mume wake ikiwa (1) mume akataa kishupavu kutegemeza familia yake, (2) yeye ni mjeuri sana hivi kwamba afya na uhai wa mke umo hatarini, au (3) upinzani wake wa kupita kiasi hufanya isiwezekane kwa mke kumwabudu Yehova.—1 Wakorintho 7:12, 13.

7. Ni lazima wenzi wa ndoa wawe waaminifu kwa mmoja na mwenzake. Uzinzi ni dhambi dhidi ya Mungu na dhidi ya mwenzi wa mtu. (Waebrania 13:4) Mahusiano ya kingono nje ya ndoa ndio msingi pekee wa Kimaandiko kwa talaka inayoruhusu mtu aoe au aolewe tena. (Mathayo 19:6-9; Warumi 7:2, 3) Yehova huchukizwa wakati watu wanapotalikana bila misingi ya Kimaandiko na kuoa au kuolewa na mtu mwingine.—Malaki 2:14-16.

sam mbogo said...

Amina.kaka s

Rachel Siwa said...

Pia kashfa,dharau, maneno/Gubu, kulalamika,kutokuwa na shukrani, umimi na....Wanawake wengi wamekuwa chombo cha kustarehesha tuu, Wanaume wengi hawana mapenzi ya kweli ..Mungu wabariki wanawke

Simon Kitururu said...

:-(