Thursday, September 1, 2011

Picha ya wiki:- Kuelekea miaka 50 ya Uhuru!!!!




Sijui itakuwa hivi mpaka lini? Maana sasa tunaelekea miaka 50 ya uhuru lakini hali ni ile ile......sijui mwenzangu mnasemaje??

4 comments:

sam said...

Kwa kweli,ukisikia kujisahau ndo huku.miaka 50 ya uhuru,kwa kipengere hiki cha picha uliyo itoa hakika ni aibu.upande wa elimu nafikiri kuna tatizo wahusika hawajajipanga sawasawa,pia hawana jipya katika elimu.serikali nayo haijuwi inataka nini katika kuikomboa tanzania kielimu,huko mijini kuna utitiri wa shule za kufundisha kiingereza,ambazo wengi ya watanzania wenye kipato,huwa peleka huko,watoto wao na miongoni mwao ni viongozi hao hao walio pewa dhamana kusimamia elimu nchini.utakuta hawafuatiliiya kijijini, na shule za, chini ya mti ama kama hiyo ulio tutolea picha. ukweli,mtoto kujuwa kiingereza/kuzungumza ,siyo ndiyo anaakili,ni lugha tu hiyo.sasa huo ndo mtazamo wa wengi tanzania na ndiyo maana vishule vya kiingereza viko vingi,visivyo ha na ubora.kwahiyo katika miaka50 ya uhuru,sura ndo hiyo kwa elimu,na maisha kwaujumla. kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Unajua kinachonisikitisha mimi zaidi? Kuona hivyo vishule vya kiingereza vikifunguliwa vingi ili watoto wa wenye pesa wasoma wakati hawana akili. Na baya zaidi wakati hawajui hata kiswahili. Je kwanini wasianzishe mashuleni kufundisha lugha za asili basi...yaani hii inaniuma sana sana ... Halafu sasa walimu wanaoajiliwa mamaaa weeee... si afadhali sasa wangejenga hizo shule na kuwaboresha hao walimu zaidi kwa kiswahili na kufundisha KISWAHILI kwanza?....Samahani lakini nimechukia sana...

sam said...

Umesema yaliyo kuwa akilini mwangu. maarifa yanapatikana kwa lugha ulio izowea.mimi ni mswahili,huku niliko,kiingereza siyo lugha ya ngu ya kwanza.sasa nilazima kwa kila jambo nalo lifanya,litakalo husisha kiingereza, huanza kiswahili kwanza,nitakapokuwa na uhakika kwa lugha yangu ya kiswahili,english inafuata,nahii ndiyo jambo la muhimu,kwetu sote wenye lugha ya kwanza kiswahili. sasa una kuta kiswahili chenyewe watoto hawakijuwi,sembuse,kiinglishi!.mimi watoto wangu tukiwa bongo nawaomba nduguzangu wawaongeleshe kiswahili,kwa sabau wana sikia,na haina haja ya kukaa unapiga kiingereza wakati waliomzunguka wote kiswahili ndo lugha yao ya kwanza. haya bibie tuwaachie na wengine,wanasemaje. kaka S

emu-three said...

Wakti mwingine nawaza huenda ni mpango ulipangwa kwa ule usemi kuwa ukitaka kuwatawala watu hakikisha kuwa `hawaerevuki' na njia mojawapo ni kutokuwapatia nafasi ya elimu...
Shule nzuri ni gharama kubwa na waneye uwezo ni hao hao, zimeanzishwa shule za kata, hazina walimu, zipo sehemu ambapo hakuna usafiri...mazingira magumu...hata walimu wenyewe hawavutiki kwenda huko...hizo ni shule za kata ukizungumzia sekondari..sasa shule za masingi ambazo ndio msingi wa elimu, zipoje?
Elimi ni muhimili wa maendeleo, ingelitakiwa kila mbunge, kila kiongozi azijue shule ake zote, mazingira yake na kuziweka hewani, zijulikane, hili ni rahisi sana kwasababu kuna viongozi wa kata, kuna watendaji..kwa ujumla hatupo makini kwa hili, viongozi hawapo makini kwasababu hawana shida, toka lini aliyeshiba akawa anajua njaa ilivyo?