Monday, September 19, 2011

MIAKA 50 YA UHURU TANZANIA

NGOJA TUANZE WIKI NA WIMBO HUU!!!

SWALI HIVI TUPO HURU KWELI? NA KWELI TUNA AMANI ? HAYA JUMATATU NJEMA NDUGU ZANGU.....

8 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

ni kweli kama uhuru ni neno uhuru si uhuru wa kufaidi matunda huru wa kulala na kuamkatuu upo ila hauna uhakika wa kuwa kesho ukiamka utaishije kwani kwa sisi watz hakuna mtu atakuambia leo hii litokee jambo la kukaa siku nne bila kwenda popote basi hali itakuwa mbaya kwani hamna mwenye akiba ya pesa wala chakula ndani hii si mzura kimaisha kwani tunaishi kama kuku wa kienyeji wale anaofuga nzee mapunda au mbogo na rafiki yake chiume pale ziwani kuwa akitoka asubuhi ni kwenda kupapaa maporini ili ashibe na huku mwewe akimyemelea ndo maisha yetu wa tz na miaka 50 hii ni kwelihuru na amani ipo ila huru na amani kweli bila shibe huo si huru wala si amani kwani ndo utaslkia kila siku yule kavunjiwa kule moto yote haya ni matokeo ya huru na amani bila vitendea kazi mada ni mzuri kiasi

Simon Kitururu said...

Mmmh!
Jumatatu njema kwako pia Kapulya!

EDNA said...

Dada Yasinta swali zuri,ila jibu la hili swali linategeamea na tafsiri ya mtu juu ya neno lenyewe "UHURU"

Rachel Siwa said...

Duhhh Uhuru,Amani, Tanzania, Afrika, ndiyo kwetu, sijui tumepata au tumepatikana Nawazaaaaa!!!!Mungu ibariki Tanzania.

emu-three said...

Kweli uhuru inatafsiri pana, na hapa kwetu viongozi wana nadi hivyo kuwa tuno uhuru....sawa kwasababu hatuitwi kuwa tunatawaliwa na ukoloni, kwamba hakuna bendera ya nchi nyingine kuwa sisi ni `koloni la...' lakini kweli uhuru huo tunao...
Uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe, una slimia gani hapa kwetu,sidhani kuwa ni 100 kwa mia, hebu angalia sakata la ugaidi, na mengineyo, ambayo tunaamuliwa toka majuu..huo ni mfani tu, kuna bei za vyakula tunazouza nje tuaamulia na wakubwa, nk
Amani ni nini amani ni ile tu ya kuishi bila kupigana,...hapo nami nawaza kwa undani, maana kama unatoka ndani hujui utaishije, hujui utafikaje kazini, hujui hatima yako,....na ikifika usiku giza, wanaamua leo tuwashe hapa au hapa na huku umeshalipa hela yako ya LUKU, na maana yake umeshalipa hata kodi....huo ndio uhuru.
Ni kweli kuna ambyao yamepatikana, lakini ni madogo ukilinganisha na hali halisi, watu wengi wameneemeka kinyemela, ...kila siku nikipita iliyokuwa ikiitwa Pugu road natamani kulia, maviwanda yaliyokuwa yameanzishwa enzi hizo, yamegeuka magofu na sasa wanayamilikisha kwa watu wambao hawana malengo mema na yaliyokusudiwa...nakikumbuka sana kiwanda mama cha NECO...kilikuwa kiwanda cha chuma, ...viwanda kamahivi vilitakiwa kuboreshwa na nguvu ikawekwa hapo, kwani kwa kiwanda kama hicho, tunapata pesa za kigeni, angali Mgololo...oooh, kila nikiwaza nasikitika na kusema sasa changamoto la miaka 50 ni kama kibanda cha baba ynagu alichojenga cha kuanzia maisha alihamia kikiwa hakijakamilka na sasa kinabomoka hajikamalika...na hata uwezo wa kukikarabati hakuna maana hata sisi watoto wake tunabangaiza tu, kuganga njaa...hiyo hela ya kukikarabati itatoka wapi, labda tukimilikishe tugeuke tuwe watumwa.
wakatabahu emu-three

Salehe Msanda said...

Habari.
Sisi tupo huru na tuna amani,tatizo tunashindwa kutoa tafsiri ya neno uhuru na amani na kisha kuifanyia kazi hicho kitu kinainachoitwa amani na uhuru.

Wengi tafsiri ya uhuru na amani hasa kwa sisi watanzania tunadhani ni kukaa tu bila ya kuwajibika hasa katika nagazi ya familia.

Kila la kheri.

Anonymous said...

Hatuko huru siunaona nilivyojishika kwenye picha hiyo? inaashiria nini?
hiyo ni style lakini siyo kivile.

Yasinta Ngonyani said...

Shukrani, Shukrani wote kwa mchango wenu...nimeusikiliza wimbo huu tena na tena na ninachosikia kwenye masikio yangu ni haya maneno matatu UHURU, AMANI NA UPENDO KWAMBA TANZANIA TUNASIFIKA...kwa ninavyofahamu mimi:-
Neno UHURU= NI HALI YA KUTOTAWALIWA NA MTU MWINGINE, PIA NI HALI YA KUFANYA MAMBO BILA KUINGILIWA KATI.

Neno AMANI= NI HALI YA USALAMA,YAANI KINYUME CHA GHASIA AU FUJO AU VITA KUWA NA UTULIVU.

NA NENO UPENDO= NI ILE HALI YA KUPENDANA AU NAWEZA KUSEMA JINSI YA KUPENDANA...Sasa nimejiuliza je kuwa hivi tu kwa mtanzania kunatosha? au sijui nakologa tongwa?